- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wanawake wa Kichina Waandamana Kupinga Kombe la Dunia

Mada za Habari: Asia Mashariki, China, Maandamano, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia
12 women staged an anti-World Cup protest on 7 of July in Shanghai. Photo from Weibo via Offbeat China. [1]

Wanawake 12 walifanya maandamano ya kupinga kombe la dunia tarehe 7 Julai jijini Shanghai. Picha na Weibo Offbeat China.

Offbeat China alieleza kwa nini wanawake hao wana hasira na jinsi Kombe la Dunia linavyoharibu mahusiano ya kifamilia nchini China.

Wanapinga mambo mawili makubwa: 1) wapenzi wao kupuuza majukumu yao ya kifamilia kwa sababu ya kuangalia mpira usiku wa manane; 2) tabia za kucheza kamari kwa mashindano hayo.