Pongezi Kemkem kwa Alexander Sodiqov Kutoka Toronto, Canada

Posti hii ni sehemu ya kampeni yetu ya #FreeAlexSodiqov: Mwandishi wa GV aliyetiwa kizuizini nchini Tajikistan. 

Ni muda wa wiki tatu tangu mwandishi wa Global Voices Alexander Sodiqov kukamatwa mjini Khorog, Tajikistan, mke wake, Musharraf, amemwona mara moja tu. Ingawa imedhaniwa kwamba Alex – aliyekuwa anafanya utafiti wa kitaaluma wakati wa kukamatwa kwake – anashitakiwa chini ya kifungu cha 306 (uhaini) hapajawa na taarifa yoyote ya wazi kwa tukio hili kutoka mamlaka ya Tajik. Alex ni msomi, sio mpelelezi.

Igor

Igor Shoikhedbrod anazungumza katika tukio kwa ajili ya Alexander Sodiqov. Picha kwa hisani ya freesodiqov.org, tovuti iliyoanzishwa na wenzake Sodiqov katika Chuo Kikuu cha Toronto.

Global Voices imekuwa ikiripoti, kila inavyowezekana, mikutano ya kitaaluma inayofanyika kumuunga mkono Alex Sodiqov. Ziko hapa, hapa, hapa na hapa. Kwa ujumla kulikuwa na mikutano kumi na mbili iliyofanyika kwa niaba ya Alex. Juni 27 kulikuwa na mkutano uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Toronto nchini Canada, mahali ambapo Alex ni mwanafunzi wa Shahada ya Uzamifu (PhD) na mhadhiri msaidizi. Mwanzoni mwa mkutano – sasa katika muundo unaopatikana kirahisi – Igor Shoikhedbrod, mwanafunzi mwenzake wa shahada ya uzamifu katika Chuo Kikuu cha Toronto, alimsifia Alex, si tu kama mwenzake, lakini kama rafiki wa familia ya Sodiqov:

Alex anajua mengi kuhusu historia ya Tajikistan utamaduni wake na taasisi zake. Na anajua mambo haya si kama mtu anayetazama kutoka nje, lakini kama mtu mwenye uzoefu wa taasisi hizo, historia hiyo na utamaduni huo. Mbali na kuwa mashuhuri katika masomo, Alex, kwanza kabisa ni mtu apendaye familia. Nakumbuka wakati mmoja nilimuuliza alivyokuwa anajisikia asubuhi wakati tukiwasilisha kazi na yeye alisema kwamba alikuwa hajalala kwa sababu alikuwa amempeleka mke wake na mtoto wake Erica hospitalini kwa sababu ya homa ya kuota meno. Alex hakukaa kwa muda katika idara kwa sababu alitaka kutumia muda wote aliokuwa nao na mke wake na binti. Moja ya sababu Alexander alikuwa nchini Tajikistan [alipokamatwa] mbali na maslahi yake kitaalamu katika eneo hilo, ilikuwa kwa sababu [kama ilivyo kwa wahadhiri wengine wasaidizi] mkataba wake ulikwisha mwezi Aprili na alihitaji kufanya kazi kujiongezea kipato kwa ajili ya familia yake wakati wa msimu wa kiangazi. Mara ya mwisho nilizungumza na Alex na familia yake na alinipikia chakula halisi cha Tajik kiitwachoplov na aliahidi kuniletea kazan (sufuria) kama zawadi kutoka Tajikistan. Ni matumaini yangu kwamba anaweza kuachiliwa bila kuchelewa na kwamba ataweza kuunganishwa na familia yake. Tunahitaji wasomi zaidi nchini Tajikistan kama Alex.

Sehemu nyingine ya mkutano waweza kuitazama hapa:

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.