- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

PICHA: Wapelestina Wanatufundisha Namna ya Kuishi

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Israel, Palestina, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

Mpalestina Sayel anatwiti kwa wafuasi wake 1,800 kwenye mtandao wa Twita picha ifuatayo ya wakazi wa Gaza wakipanda maua kwenye maganda ya silaha za Israeli. Anasema:

Wapalestina wa Gaza wanapanda maua kwenye maganda ya silaha yanaokotwa kwenye nyumba zao zinazoshambuliwa na Israel. Tunafundisha namna bora ya kuishi!

Leo ni siku ya 19 ya mashambulizi ya Israel kwenye makazi ya Wapalestina, ambayo yamepoteza maisha ya watu wasiopungua 1,000 na kujeruhi wengine 6,000.