Habari kutoka Julai, 2014
Kuhusu Kuwa Kijana, Mweusi na Mgeni nchini Afrika Kusini
Leila Dee Dougan anaweka video ya muziki inayotoka kwenye toleo la hivi karibuni la msanii wa Afrika Kusini Umlilo: Umlilo (ambaye hapo awali aliandikwa kwenye tovuti ya Africa is a Country) anaendelea kupunguza mipaka ya kijamii, akivunja vunja mila zinazohusu masuala ya jinsia na mapenzi kwa kutumia albamu yake ya...
Haki za Mashoga Zaendelea Kudaiwa kwa Kasi Nchini Cuba
Maandamano ya pili ya "besada" ambapo watu hukaa na kubusiana, yalifanyika kupinga sheria mpya kazi nchini Cuba, inayoondoa utambulisho wa jinsia kuwa aina ya unyanyapaa kazini.
Ajentina Yaichapa Uholanzi, Kukutana na Ujerumani Kwenye Fainali za Kombe la Dunia
Ajentina ilitinga katika fainali za kombe la Dunia kwa mara ya mwisho mwaka 1990 na ikapoteza kwa Ujerumani Magharibi, na hiyo inaufanya mchezo wa Jumapili na Ujerumani kuwa historia inayojirudia baada ya miaka 24.
Ajentina Yafurahia Mpinzani Wake wa Jadi Brazil Kuchapwa Vibaya na Ujerumani
Bendi ya Jeshi Alto Peru Mounted Fanfare Band ilipiga wimbo wakati wa gwaride la Siku ya Uhuru kwa kuchanganya na mashairi yenye vijembe kwa watani wao Brazili kukumbuka walivyowachapa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1990.
Mwanamke wa Ivory Cost Aangushwa Kutoka Ghorofa ya Sita kwa Kudai Mishahara yake
Msichana mwenye asili ya Ivory Coast alipoteza maisha kutokana na kile kilichotaarifiwa kuwa alisukumwa na mwajiri wake na kuanguka kutoka ghorofa ya 6 ya jengo kwa kile kinachodhaniwa kuwa ni ugomvi baina yao kuhusiana na malipo ya mshahara wa msichana huyo.
Waandishi wa kimataifa Wakashifu Israeli kwa Kuendelea kwa Ujenzi wa Makazi
Waandishi kumi na sita wa kimataifa ambao walishiriki katika Tamasha la Wapalestina la Fasihi, lililofanyika katika miji kadhaa Palestina kuanzia Mei 31 hadi Juni 5, walitoa taarifa kukashifu Israeli kwa kuendelea kwa ujenzi wa makazi na kupongeza juhudi za kususia kampeni ya Boycott Divest and Sanction (BDS). Taarifa, kupitia mtandao...
Baada ya Kuchoshwa na Kudorora kwa Uchumi, Wa-Ghana Waanzisha Harakati
Hali ya ghadhabu dhidi ya serikali ilitokana na ongezeko la haraka la kushuka kwa thamani ya fedha ya Ghana pamoja na kukosekana kwa mafuta vituoni hali iliyopelekea kuwa na misururu mikubwa ya watu katika vituo vya mafuta ya petroli
Pongezi Kemkem kwa Alexander Sodiqov Kutoka Toronto, Canada
Posti hii ni sehemu ya kampeni yetu ya #FreeAlexSodiqov: Mwandishi wa GV aliyetiwa kizuizini nchini Tajikistan. Ni muda wa wiki tatu tangu mwandishi wa Global Voices Alexander Sodiqov kukamatwa mjini Khorog, Tajikistan, mke wake, Musharraf, amemwona mara moja tu. Ingawa imedhaniwa kwamba Alex – aliyekuwa anafanya utafiti wa kitaaluma wakati...
Mfungo wa Ramadhani Wawaingiza Watu Matatani kwa Kula Daku Usiku Nchini Misri
Vijana kumi na moja walikamatwa nchini Misri wakiwa wanapata daku usiku, kitendo kinachochukuliwa kuwa kosa la kukutana usiku kinyume na sheria. Noor Mattar ana taarifa zaidi kuhusu mahabusu hao wa 'kosa la kula daku' kinyume cha sheria.
Kuongozeka kwa Vitendo vya Kujichukulia Sheria Mkononi Nchini Senegali
Sada Tangara, mpiga kura na mwanablogu anayeishi Dakar, nchini Senegali aliweka picha-habari inayohusu kuongezeka kwa matukio ya kujichukulia sheria mkononi kwenye mitaa ya Dakar, mji mkuu wa Senegali. Anaeleza mwanzo wa mradi wake na kwa nini aina hii maarufu ya haki imeshika kasi jijini Dakar [fr] : Il faut savoir...