- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Namna Teknolojia Inavyosaidia Watu Kujifunza —na Hata Kuokoa—Lugha za Dunia

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika Kusini, Asia ya Kusini, Marekani ya Kaskazini, Nchi za Visiwani, Ulaya Magharibi, Australia, Brazil, China, El Salvado, India, Ireland, Kanada, Kenya, Mali, Marekani, Norway, Paraguai, Uhispania, Uzbekistan, Harakati za Mtandaoni, Lugha, Uandishi wa Habari za Kiraia, Sauti Chipukizi
Kenkyusha’s New Japanese-English Dictionary by Niko Kitsakis (CC-SA-3.0)

Kamusi mpya ya Kijapani na Kiingereza iitwayo Kenkyusha [1] picha na Niko Kitsakis (CC-SA-3.0)

Makala haya yameandikwa na mwandishi mwalikwa Allyson Eamer, mwanazuoni katika kitivo cha stadi za jamii na lugha katika Taasisi ya Teknolojia ya Chuo Kikuu cha Ontario. Toleo la makala haya  lilichapishwa awali [2] kwenye blogu ya Mradi wa Ethnos.

Moja wapo ya lugha zinazopotea kwenye sura ya dunia hufa kila baada ya siku 10 hadi 14 [3]. Katika jitihada za kuziokoa lugha hizi zisipotee, wasemaji, wanazuoni na wataalamu wa Teknolojia wanaungana kuchungua namna teknolojia za kidijitali zinavyoweza kutumiwa katika kuhuisha lugha. 

Lugha zimekuwa katika hatari ya kupotea kadri muda unavyokwenda na kadri wazungumzaji wake wanavyohamia kwenye lugha nyinginezo zinazoonekana kuwa na nguvu ya kisiasa na kiuchumi. Mara nyingi, mabadiliko hayo hutokea kwa sababu ya ajenda za kikoloni za kujitanua ambazo huwafanya wenyeji, tamaduni, na ardhi zikitekwa na wajenzi wa falme zao. 

Katika hali inayotia matumaini, baadhi ya wasomi hawafurahishwi na kile kinachoweza kuitwa “Ku-Darwinishwa kwa lugha”, au kubaki kwa lugha zenye nguvu na kupotea kwa zile zisizo na nguvu. Hoja yao kuu ni: Je, si rahisi ste tukizungumza lugha moja?

Sitafafanua namna kila lugha ilivyo na tofauti za kipekee kwenye mtazamo wa kidunia: namna msamiati wa lugha unavyoofunua tunu za watu wanaoizungumza, namna maarifa ya asili yanavyobebwa katika muundo wa lugha, na namna sanaa, kujieleza, historiam utamaduni, uchumi na utambulisho vinavyofungamanishwa na lugha. Badala yake ninaendelea kwa imani kwamba, kama nilivgo mimi, wewe ndugu msomaji unaamini kwamba kupotea kwa lugha ni janga na kwamba wenye lugha hizi za asili duniani kote wameshuhudia wakinyang'anywa vingi.

Miniature DNF Dictionary  by Tomasz Sienicki (CC-SA-3.0)

Kamusi ndogo ya mfumo wa DNF [4]picha na Tomasz Sienicki (CC-SA-3.0)

Teknolojia inaweza kuwaunganisha walimu na maudhui ya lugha na watu wanaotamani kujifunza lugha hizo duniani kote kwa wakati ule ule. Teknolojia inaweza kuhifadhi lugha zilizokwenye hatari ya kupotea kwa kutumia mfumo wa sauti. Inaweza kutengeneza na kusambaza mitaalama na zana za kujifunzia kirahisi na kwa wepesi. Inaweza kurahisisha kujifunza kwa kujitegemeea kupitia michezo, kupakua programu na viwezeshi vingine. Ianweza kuwaunganisha walimu na wanafunzi wa lugha kwa namna mbalimbali.

Watu wenye fikra za kuleta mabadiliko wanaunganisha nguvu za kiteknolojia kuzileta lugha kutoka kwenye hatari ya kupotea, na katika hali nadra sana, kuzifufua lugha zilikwisha kufa.

Hapa ni pitio fupi la namna mbalimbali ambazo teknolojia ya kidijitali zinavyotumiwa katika jitihada hizi:

Ulaya

Marekani Kaskazini

Afrika

Marekani ya Kati na Kusini

Asia

Ncha ya Kaskazini

Mashariki ya Kati

Nchi za Bahari ya Pasifiki

Kwa habari za karibuni zaidi kuhusu teknolojia kuhusu matumizi ya elimu ya lugha za asili, angalia kwenye tovuti ya hifadhi ya maudhui [25] ya Allyson Eamer