- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mwanamke wa Ivory Cost Aangushwa Kutoka Ghorofa ya Sita kwa Kudai Mishahara yake

Mada za Habari: Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini, Cote d'Ivoire, Lebanon, Habari za Wafanyakazi, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia

Koaci.com [1] aliye na maskani yake huko Ivory Coast aligundua kuwa msichana wa Ivory coast alikutwa na mauti kwa kile kinachosadikiwa kuwa alitupwa kutoka ghorofa ya 6 kutokana na ugomvi kati yake na mwajiri wake, ugomvi unaosadikiwa kusababishwa na mwajiri wa msichana huyo kutokumpa mishahara yake.

Carolle Feby anataarifu katika mtandao wa Koaci.com kuwa [fr]:

Une jeune Ivoirienne est morte Rechercher morte après avoir été poussée du 6ème étage d’un immeuble par son patron pour lui avoir réclamé son salaire à Beyrouth au Liban.
Les faits ont été rapportés à koaci.com par un jeune camerounais, après les révélations de sa sœur voisine de la victime.
Une jeune fille d’une vingtaine d’années de nationalité ivoirienne a été retrouvée morte en bas de son immeuble.
Selon la voisine de la jeune infortunée dont le nom n’a pas été révélé, la fille aurait été poussée du 6ème étage d’un immeuble à Asharfir, un quartier de la ville de Beyrouth au Liban, le mardi 1er Juillet par son patron.
Elle lui réclamait son salaire et l’homme qui a été manifestement contrarié par cette requête, l’aurait poussée sous l’effet de la colère.
Cette jeune expatriée aurait quitté la Côte d’Ivoire depuis des années pour aller travailler en tant que servante au Liban, comme beaucoup de jeunes Ivoiriennes.
Les histoires plus ou moins dramatiques d'Ivoiriennes travaillant au Liban sont malheureusement légions.
Il y a quelques mois, après une révélation de koaci.com un groupe d'africaines avait été rapatrié du Liban après avoir réussi à échapper à leurs patrons qui leurs faisaient subir des sévices corporels et moraux.

Msichana wa Ivory Coast mwenye miaka inayokadiriwa kufikia 20 alikutwa amefariki kwa kile kilichoripotiwa kuwa alisukumwa na kuanguka kutoka ghorofa ya 6 pale alipokuwa akidai mshahara wake huko Beirut, Lebanon.
Taarifa hii ilitolewa katika mtandao wa Koaci.com na msichana mmoja wa Cameroon kutokana na ushuhuda alioutoa dada yake ambaye ni jirani wa msichana aliyefariki.
Kwa mujibu wa jirani yake, ambaye jina lake limehifadhiwa, msichana huyo alisukumwa na kuanguka kutoka ghorofa ya 6 ya jengo lililopo huko Asharfir – Agalizo: Bila shaka alikuwa anamaanisha Achrafieh -, jirani na jiji la Beirut huko Lebanon siku ya Jumanne tarehe 1 Julai.
Alikuwa akidai mshahara wake, mwanamume huyo alikataa, na ndipo kwa hasira, alimsukuma msichana huyo.
Msichana huyu aliyeishi nje ya nchi yake kwa miaka mingi, habari zinasema kuwa alitoka Ivory Coast miaka kadhaa iliyopita kwa ajili ya kufanya kazi za ndani nchini Lebanon, jambo ambalo limekuwa la kawaida kabisa kwa wasichana wa Ivory Coast.
Matukio ya aina hii kwa bahati mbaya yamekuwa ya kawaida sana nchini Lebanon.
Miezi michache iliyopita, mara baada ya Koaci.com kuweka bayana kuwa kundi moja la wanawake wa kiafrika kunyanyaswa walifanikiwa kurudishwa nchini mwao salama kutoka Lebanon.

Kwa habati mbaya, matukio haya yamekuwa ya kawaida sana nchini Lebanon pamoja na nchi nyingine za kiarabu wanaotunmia mfumo wa Kafala, au mfumo wa ‘Ufadhili’. Kama inavyofafanuliwa na shirika la kutetea haki za binadamu katika taarifa ya mwaka 2014 ya Lebanon [2]:

Sheria ya kazi haiwahusu wahamiaji wanaofanya kazi za ndani na badala yake wanakabiliwa na taratibu kali za uhamiaji chini ya mfumo wa mwajiri-mfadhili mahususi- mfumo wa kafala- mfumo unaowaweka wafanyakazi katika hatari ya kukandamizwa na kudhalilishwa. Wakati waziri wa Kazi aliyemaliza muda wake, Charbel Nahhas Januari 2012 alitangaza kuwa angeangalia uwezekano wa kufutilia mbali mfumo wa kafala,mwaka 2013, waziri wa kazi, Salim Jreissati alishindwa kufanya hivyo au kuweka sheria ambayo ingewalinda zaidi ya wafanyakazi wa ndani wanaokadiriwa kufikia 200,000 nchini humo. Mwezi Julai, mahakama ya makosa ya jinai ilimuhukumu mwajiri mmoja kifungo cha miezi sita gerezani, kutozwa fidia, na kutakiwa kulipa fidia ya uharibifu pamoja na kulipa mishahara ya mfanya kazi wake wa ndani ambaye hakuwa amemlipa kwa miaka kadhaa. Matukio ya wahamiaji wanaofanya kazi za ndani kuwashitaki waajiri wao kwa kuwadhalilisha yanazidi kushika kasi, hata hivyo, wanakabiliwa na changamoto za kisheria na hatari ya kuwekwa gerezani na kurudishwa makwao kutokan na mfumo kandamizi wa taratibu za uhamiaji.