Mitandao ya Kijamii Yasaidia Kuikoa Côte d'Ivoire Iliyokumbwa na Mafuriko

Abidjan na maeneo mengine ya Côte d'Ivoire yamekumbwa na mafuriko makubwa katika majuma kadhaa yaliyopita [fr]. Wakazi wa maeneo husika walijipanga kwenye mitandao ya kijamii ili kusaidia namna ya kuwaokoa wananchi waliokuwa wamekwama kwenye janga hilo. Kwenye mtandao wa twita na facebook, #CIVSOCIAL ilikuwa ni alama ishara iliyokuwa ikitumika kwa ajili ya shughuli za uokoaji wa dhararua na misaada ya kibinadamu. Ilianzishwa mwaka 2011 wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi na ikazinduliwa kwa mara nyingine tena wakati mafuriko yaliyoikumba Abidjan na nchi hiyo yote. Ukurasa wa facebook wa CIVSOCIAL ulitumika kukusanya picha, video na shuhuda pamoja na michango kwa kila eneo lililoathirika. Hapa unaweza kuona video ya moja wapo ya maeneo yaliyoathirika na mafuriko :

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.