Mwaka umepita tangu kung'olewa madarakani kwa rais wa Misri Mohamed Morsi na serikali mpya tayari inakosolewa vikali kwa uvunjifu wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na kukamatwa kiholela kwa raia.
Sheria mpya ya Misri ya kudhibiti mikusanyiko ndiyo hasa imewasha hasira kali miongoni mwa Wamisri, wengi wakijaribu kupinga sheria hiyo lakini hatimaye kujikuta wakikamatwa wao wenyewe, ikiwa ni pamoja na baadhi ya wanaharakati maarufu kama vile Alaa Abd El Fattah, aliyehukumiwa kifungo cha miaka 15 jela mwezi uliopita, kwa ajili ya kuandaa maandamano pasipo kibali.
Kwa siku za kwanza za mwezi wa Ramadhani, mwezi mtukufu wa kufunga kwa Waislamu, vikosi vya polisi vilivamia makazi ya watu na kuwakuta vijana 11 wakipata daku (chakula cha usiku kinacholiwa na Waislamu kabla ya kuendelea na mfungo kwa siku inayofuata), shughuli ambayo inapofanywa na kundi la watu, huonekana kukiuka sheria ya mkutano kama baadhi yao walivyobashiri. Raia mtandaoni walianzisha alama ashiria #معتقلي_السحور [ar], ambayo tafsiri yake ni wafungwa wa daku.
Ahmad Abd Allah aliandika kwenye ukurasa wake wa Facebook yafuatayo [ar]:
١١ واحد بيتسحروا في بيت واحد منهم في دمنهور … الداخلية قبضت عليهم بتهمة التظاهر من غير تصريح … الحرية لمعتقلي السحور
Watu kumi na moja walikuwa wakipata daku usiku katika moja ya nyumba zao. Wizara ya Mambo ya Ndani iliwakamata kwa tuhuma za kufanya mkutano haramu … waachilie huru wafungwa wa daku
Mtumiaji Twita Mohamed Hazem, kutoka Damnhour, alitwi kuwaunga mkono marafiki zake:
مش عارف ابكي علي مجزرة الحرس الجمهوري
ولا ابكي علي اصحابي 11 المعتقلين
حسبي الله ونعم الوكيل
#معتقلي_السحور
— Mohamed Hazem (@HazeemZZ) Julai 5, 2014
Sijui kama mimi nilie kwa sababu ya mauaji yaliyofanywa na walinzi wa serikali au shauri ya rafiki zangu 11 walioko kizuizini
Kwa kejeli baadaye alitwiti:
ياتري ياوكيل النيابة هتعمل الاحراز جبنة رومي وزتون
ولا هتخليها مولوتوف
#كل_هدفهم_انهم_يصوموا #معتقلي_السحور :(
— Mohamed Hazem (@HazeemZZ) Julai 5, 2014
Je, Wakili wa Serikali atatumia ushahidi wa vyakula vya maharage na mizaituni waliyokutwa nayo?
Na Shahdan-shosh alitwiti picha ya wafungwa hao 11 na kubainisha :
التهمة سحور جماعي
حيازة فول وفلافل وزبادي #معتقلي_السحور pic.twitter.com/2cbVqvTsrl
— Shahdan (@Shahdan_shosh) Julai 5, 2014
Kosa lao hasa ni hili: Kundi la suhoor. Walikamatwa na (maharage) machafu, falafel na jibini katika nyumba waliyokutwa.
Mwanaharakati Wael Abbas alitwiti kwa wafuasi wake 265000:
انا غالبا هالغي حفل الفطار السنوي اللي باعمله كل سنة في بيتي احتراما لقانون التظاهر الجديد :) #قبضوا_عليهم_وهم_بيتسحروا #دمنهور
— Wael Abbas (@waelabbas) Julai 4, 2014
Itanibidi pengine mimi kuachana Iftar [chakula maarufu cha swaumu] yangu ya kila mwaka kutii sheria mpya ya maandamano)
Aliongezea:
اصلا نص اللي كانوا عندي في الفطار السنة اللي فاتت يا محبوسين يا هربانين يا مطاردين :)
— Wael Abbas (@waelabbas) Julai 4, 2014
Hata hivyo, nusu ya wale ambao mimi niliwaalika kwa ajili ya Iftar mwaka jana wako jela, uhamishoni au ni watuhumiwa wa makosa ya jinai)
Mwaka jana, serikali ya Morsi ilijaribu kulazimisha matumizi ya sheria kama hiyo inayozuia mikusanyiko ambayo hata hivyo, haikufaulu baada ya kilio kutoka mashirika ya kimataifa. Blogu ya Misri WikiThawra [ar], ambayo inaendeshwa na Kituo cha Misri cha Uchumi na haki za Kijamii inadai kuwa watu wasiopungua 80 wamefariki wakiwa chini ya ulinzi katika kipindi cha mwaka mmoja na zaidi ya watu 40,000 wamewekwa kizuizini au wako kwenye mashitaka katika kipindi cha mwenzi Julai 2013 (kuiondoa serikali ya Morsi) na katikati ya Mei 2014.