- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mambo Matano Unayopaswa kuyajua Kuhusu Harusi za Kitukimeni

Mada za Habari: Turkmenistan, Sanaa na Utamaduni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia
Image of a Turkmen bride (screenshot taken from a YouTube video uploaded by Basim Annanow)

Picha ya bibi harusi wa Kituruki. Picha imepigwa kutoka kwenye video ya YouTube iliyowekwa na Basim Annanow

Ýigit çal söýgi sazyňy,

Gelin artdyr sen näziňi

Oýnaň şadyýan tansyny çünki bugün toý toý

Aýdalyň biz toý aýdymy, bugün bizde toý toý 

Kijana hucheza muziki wa mapenzi, 

Bibi harusi huchepuka kidogo, 

Cheza kwa furaha kwa sababu ni siku yako ya harusi, 

Tutaimba wimbo wa harusi yetu,

Leo tunasherehekea.

Harusi ni za muhimu sana kwa kwa Watukimen. Kuoza watoto wao huonyesha mwendelezo wa maisha ya kijamii na thamani ya familia kwenye jamii. Kiasili Waturukimeni wana familia kubwa na harusi ni fursa ya kuona ndugu wnegi zaidi, dalili ya heshima kwa majirani.

Kuna mila kadhaa za kufanya katika siku ya harusi ya Waturukimeni. Hapa ni muhtasari mfupi wa mambo ya kutazama:

1. Lazima uwe na mwimbaji maarufu! Utaenda kucheza mitaani! 

Kama una utajiri wa kutosha kukaribia kununua utajiri wa gesi asilia ya taifa hilo, unaweza kumkodisha [1] J-Lo, lakini hata kama huna utajiri huo basi angalau mwimbaji utakayempata awe na uwezo wa kuwasisimua waalikwa wako.

Hapa chini ni mfano wa uimbaji wa kwenye harusi kwa kumtumia mwimbaji maarufu wa nchi hiyo Kakysh:

Şemal näz edip öwüsýär şugün

Güller näz edip öwüsýär şügün

Ýarym näz edip ýylgyrsaň senem

Toý güni aýly günüm, sögülim şugün.

Upepo unavuma kwa kasi ya kubembeleza,

Maua yanavuma taratibu,

Mpenzi wangu utatabasamu taratibu,

Mpenzi wangu leo ni siku ya harusi yetu

Kwenye jukwaa la soga maarufu nchini Turkmenistan, Ertir.com, watumiaji walijadili mashairi ya wimbo huo.
NitrogeN Sifa [2] [tkm] Kakysh, anauliza swali kuhusu hamasa inayoonekana mara kwa mara kwenye wimbo huo:

gowy aydyaray Kakysh. Aydymlarynyng köpüsinde Läle sözi geçyär. Shondan yanan oydyan 

Kakysh anaimba vizuri. Kwenye nyimbo zake nyingi anatumia jina  Läle. Labda alikwaza kimapenzi.

Meka MerGenius pia ana jiuliza [3] [tkm] kuhusu sauti ya mtu anayeitikia wimbo huo:

Kakyş Amandurdyyew näz edyär mi?

Hivi Kakysh Amandurdyyew anachepuka?

Watumiaji wengine wa mtandao wanajadili [4] [tkm] mitazamo yao kuhusu ndoa:

oylenyancha her hili sozler aydylyar son kan aydylanok

Kabla tu ya ndoa watu husema maneno yote ya bashasha, lakini hawafanyi hivyo baada ya kuoana

NitrogeN anandelea [5], kutania [tkm]:

durmusha cykyp semreyar song shemal akidip bilenok

Wanapooana, wananenepeana, na upepo hauwezi kuwapepesua tena

2. Vazi la harusi lazima limwonyeshe bibi harusi kwa sababu baadae atavalishwa mtandop na kuufunga mdomo wake mbele ya wakwe zake.

Mavazi ya harusi nchini Turkmenistan yanatofautiana sana, yakiwa na rangi na mitindo tofauti yenye bei tofauti. Vazi la asili la Watukimeni lenye ushungi na gauni —likipambwa kwa rangi ya shaba —linaweza kuwa na uzito wa zaidi ya kilo 35.

The heavy robe makes way for a traditional white dress when things get dancy. Screenshot from a YouTube video uploaded by Andrey Kniaz.

Ushungi mzito husaidia kuonekana kwa gauni jeupe hasa wakati wa kucheza kwa nafasi. Picha imepigwa kutoka video ya mtandao wa YouTubeiliyopandishwa [6] na Andrey Kniaz.

3. Jiandae kwa picha —picha za makundi!

Turkmen families rarely fit into a single shot (Screenshot from a YouTube video uploaded by Turkmen Owazy).

Ni nadra kwa familia ya Kitukimeni kutosha kwenye picha moja. Picha ya video ya YouTube iliyowekwa na Turkmen Owazy.

4. Vilevile, hakikisha unapiga picha mbele ya Picha Rasmi ya Rais Gurbanguly Berdymuhamedov.

Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL) imeuliza [7]ikiwa utamaduni huu ni amri rasmi au mazoea tu yasiyo rasmi. Radio hiyo inawanukuu mashuhuda wanaothibitisha kuwa picha hiyo [ya Rais] ni sehemu ya sherehe rasmi ya harusi. Hata hivyo, hiyo haionekani kuwa tatizo kwa watumiaji wa mtandao wanaojadili suala hili. 

Alex anatoa maoni [7] [ru]:

всё нормально, я бы тоже сфоткался!

Ni sawa. Hata mimi nitapiga picha mbele ya picha ya Rais pia!

5. Sehemu inayosisimua zaidi ni namna sherehe yenyewe inavyoendeshwa. Bwana harusi huja kumchukua bibi harusi kutoka nyumbani kwao.

Analazimika kuonyesha huzuni yake kwa sababu anaondoka nyumbani kwa wazazi wao milele. Hii ni sehemu ya harusi yenye mguso kwa sababu ndugu wa bibi harusi huja kumuaga. Ni wakati mbaya na mzuri kwa wakati mmoja.

goodbye

Kila bibi harusi kuwaaga wapendwa wake. Picha imewekwa mtandaoni [8] na Zarina Max