- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kuhusu Kuwa Kijana, Mweusi na Mgeni nchini Afrika Kusini

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Afrika Kusini, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Muziki, Uandishi wa Habari za Kiraia

Leila Dee Dougan anaweka [1] video ya muziki inayotoka kwenye toleo la hivi karibuni la msanii wa Afrika Kusini Umlilo:

Umlilo (ambaye hapo awali aliandikwa kwenye tovuti ya Africa is a Country) anaendelea kupunguza mipaka ya kijamii, akivunja vunja mila zinazohusu masuala ya jinsia na mapenzi kwa kutumia albamu yake ya hivi karibuni iliyotoka mwezi Julai 2014. Tazama video yake ya muziki na sikiza mawazo yake kuhusu tamaduni hizo, yeye akiwa mgeni wa nchi hiyo na namna muziki ulivyofanyika kuwa uhuru wake.