Vikosi vya kijeshi vya Israeli vimeanza kuingia Gaza, baada ya siku 10 za mapigano zilizochukua maisha ya Wapalestina 200. M-Israeli mmoja aliuawa kwa shambulio la roketi kwenye eneo la Palestina. Hatua hiyo inakuja baada ya Hamas, kikundi kinachoitawala Gaza, kukataa [2] pendekezo la kumaliza mapigano lililotolewa na Misri.
Tovah Lazaroff, mwandishi wa Boston aliye katikati ya mgogoro wa Israel na Palestina, anatwiti:
It's official from Israel's PMO office, the IDF has begun to enter Gaza.
— Tovah Lazaroff (@tovahlazaroff) July 17, 2014 [3]
Ni rasmi sasa kutoka kwenye ofisi ya Waziri Mkuu wa Israel, vikosi vya jeshi vimeanza kuingia Gaza
Anaongeza:
PMO: The cabinet approved the ground operation after Israel accepted an Egypt brokered cease fire & Hamas rejected it.
— Tovah Lazaroff (@tovahlazaroff) July 17, 2014 [4]
Ofisi ya Waziri Mkuu: Baraza la Mawaziri limeidhinisha operesheni ya ardhini baada ua Israeli kukubaliana na pendekezo la Misri la kusitisha mapigano. Hamas ilikataa mapendekezo hayo
Ardhini huko Gaza, iFalasteen anasema:
Bombs everywhere in Gaza no electricity and very thing is bright from all the fires and bombs…
#GazaUnderAttack [5]
— فلسطين i (@iFalasteen) July 17, 2014 [6]
Mabomu kila mahali hapa Gaza, hakuna umeme na kuna mwanga mkali wa milipuko na mabomu…
Nonstop bombing where no where to run… Only Allah will protect you Gaza…
#GazaUnderAttack [5]
#PrayForGaza [7]
— فلسطين i (@iFalasteen) July 17, 2014 [8]
Mabomu yanapigwa mfululizo na hakuna pa kukimbilia…Mungu tu atailinda Gaza