- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Hotuba ya Ushindi ya Rais Mteule wa Indonesia

Mada za Habari: Asia Mashariki, Indonesia, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uchaguzi

Rais mteule wa Indonesia Joko Widodo or Jokowi alitoa hotuba ya ushindi [1] akitambua moyo wa kujitolea ulioonyeshwa na wananchi:

Uchaguzi huu wa rais umechochea mtazamo mpya chanya kwetu, na kwa taifa letu kwa ujumla. Uhuru wa watu na uwajibikaji wa kisiasa vinashamiri katika nyoyo za kizazi kipya. Moyo wa kujitolea uliopotea siku nyingi umerejea tena kwa ari mpya.

Na katika kutangaza “kushiriki katika shughuli za kujitolea”, Jokowi aliwaomba watumiaji wa Facebook kupiga kura [2] na kuchagua mawaziri 34 ambao wanadhani anapaswa kuwaingiza katika Baraza la Mawaziri la serikali yake.