Hivi Ndivyo Waandishi wa Kifaransa wa Global Voices Wajivyojipanga Kusoma Kiangazi Hiki

"Summer reading" via nipmuc media center - Public domain

“Usomaji wa Majira ya joto” kutoka kituo cha habari cha Nipmuc. Kwa matumizi ya umma

Majira ya joto, ama kiangazi kwa Afrika, yamewadia. Inaonekana kile kilichogeuka kuwa utamaduni duniani kote, orodha ya kusoma ni de rigueur kabla hujaachana na vifaa vyote vya kukuweka mtandaoni na kuanza kujisomea taratibu.

Kama moja wapo ya malengo yako kiangazi hiki ni kuwafahamu zaidi (au kwa mara nyingine) waandishi wetu wa Kifaransa, usihangaike sana. Bila kwenda mbali, hapa unaweza kuona mapendekezo ya vitabu kadhaa kutoka kwa waandishi wetu wa Kifaransa.     

Andrew Kowalczukalipendekeza vitabu bora kumi ambavyo viliandikwa awali kwa Kifaransa. Orodha hii imekusanywa kutoka kwenye kazi bora zaidi za hivi karibuni kutoka kwa waandishi hao. Vingi vinapatikana kwa Kingereza pia (fungua viungo kuona tafsiri): 

Alexandre Dumas – “Le Comte de Monte-Cristo” 
Charles Baudelaire – “Les fleurs du mal
Arthur Rimbaud – “Poésies
André Gide – “Les faux monnayeurs
André Breton – “Le surréalisme et la peinture”
Albert Camus – “La chute
Eugène Ionesco – “Rhinocéros
Antoine de Saint-Exupéry – “Le petit prince
Jean-Paul Sartre – “L'être et le néant
Simone de Beauvoir – “Le deuxième sexe
Michel Foucault – “L'archéologie du savoir”
Benoît Mandelbrot – “Les objets fractals: Forme, hasard et dimension”   

Hiyo tayari ni orodha ya kuchangamsha akili unayoweza kuanza nayo. Hata hivyo, kama unahitaji kitu kisichopitwa na wakati, Jane Ellis pia alipendekeza baadhi ya kazi hizo maarufua:   

Voltaire – “Candide” (Mimi bado hukirudia kitabu hiki!) 
Laurent Binet – “HHhH” (kizuri sana kwa namna nyingi)
Zola – “Thérèse Raquin” (kizuri na kiko mbele kwa wakati kama kilivyo cha Candide!).
 
Bado, fasihi ya Kifaransa ina utajiri wa waandishi wanaotoka nje ya Ufaransa. Thalia Rahme alipendekeza kitabu kutoka kwa mwandishi wa Kifaransa aliyezaliwa Lebanon Amine Maalouf. Anachukua fursa hiyo pia kupendekeza orodha ya vitabu anavyosoma mbavyo havijatoka kwa waandishi wa Kifaransa kivile, ambao ni Gabriel Garcia Marquez wa Colombia au Khaled Hosseini wa Iran:  
 
Amine Maalouf -  “Identites Meurtrieres” (kwa mtazamo wake kuhusu utamaduni wa nchi mbili); “Samarcande” (kuhusu Fasihi na ushairi wa ki-Iran ),  
Gabriel Garcia Marquez – “100 Years of Solitude”  
Khaled Hosseini – “The Kite Runner”; “1000 Splendid Suns”; “And the Mountains Echoed”

Akiendeleza orodha hiyo ya Thalia, Alison Mcmillan anapendekeza riwaya kadhaa kutoka kwa waandishi wa Asia: 

Vikram Seth – “A Suitable Boy”
Shashi Tharoor – “The Great Indian Novel”
Salman Rushdie – “Midnight's Children”
Upamanyu Chatterjee – “English, August”
Kiran Desai – “The Inheritance of Loss”

front cover art for the book A Suitable Boy - Used as fair use

Mwonekano wa mbele wa kitabu cha”A Suitable Boy.” Matumizi sahihi ya picha hii yanaruhusiwa

Claire Ulrich alipendezwa na kitabu cha “A Suitable Boy” kama kitabu cha lazima. Alipendekeza baadhi ya ushairi unaoendana na riwaya hiyo: 

Ah, ninakipenda sana “A Suitable Boy”! Nimekuja kwa namna ya ‘ushairi’ na kwa siku za hivi karibuni siwezi kabisa kuachana na Paul Eluard. Na kwa sasa ninasoma kwa mara nyingine kitabu cha maisha ya Gabriel Garcia Marquez, kiitwacho “Living to Tell the Tale” 
 
Na kwa kile kinachostahili, hapa unaweza kuona orodha yangu ya vitabu vya Kifaransa ninavyotarajia kuvisoma kiangazi hiki: 
 
Gaston Leroux – “Le Mystère de la chambre jaune”
Jean-Dominique Bauby – “Le Scaphandre et le Papillon”
Anne Roumanoff – “Le couple: Petits délices de la vie à deux”
Raymond Devos – “Matière à rire”  
Victor Hugo – “Les Comtemplations” 
 
Nawatakia usomaji mwema! Na msisahau mafuta ya kujikinga na miale ya jua!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.