Wanaharakati nchini Cuba wanaendelea “kuleta mapinduzi ya kubusiana” kuunga mkono haki za mashoga.
“Maandamano ya pili ya kukaa na kubusiana kpigania tofauti na usawa,” ambayo yaliandaliwa na Proyecto Arcoiris (Mradi wa Rainbow ambao unapingana na ubepari na kupingania uhuru), ulikusanya watu 60 kwa ajili ya besada kwenye moja ya majengo makubwa ya kibiashara jijini Havana na watu wengine wasiopungua 15 wanaotokaSagua La Grande kwenye Jimbo la Villa Clara siku ya tarehe 28 Juni.
Kwenye tukio hilo, wanaharakati walisoma barua ambayo ilitumwa na Arcoiris kwenda kwa mbunge wa Bunge la Nchi hiyo, Esteban Lazo, kupinga kuondolewa kwa utambulisho wa kijinsia na hali ya afya ya VVU vinavyoonekana kuleta hisia ya ubaguzi katika mazingira ya kazi kwenye Sheria mpya ya kazi nchini humo. Pia walikusanya saini besada.
Kihistoria jamii la Mashoga nchini Cuba imekuwa ikitengwa na kuteswa, lakini imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupambana na kupata haki za watu wanaojitambulisha kuwa mashoga na wasagaji katika miaka ya hivi karibuni. Bado, hata hivyo, kuna mengi ya kufanyiwa kazi.
Angalia baadhi ya picha hapa chini zilizopigwa kwenye maandamano hayo ya kukaa na kubusiana kwa hisani ya Rogelio Díaz Moreno na Maykel González Vivero, na kuchapishwa kwa mara ya pili kwa ruhusa yao. Kwa habari zaidi, angalia video hii hapa, “Besada kupigania Tofauti na Usawa, Havana, 2014,” na Raquel Pérez.