Dunia Yatwiti Kuwatetea Wanablogu wa ki-Ethiopia Waliokamatwa Julai 31

Free Zone9 Tumblr collage. Images used with permission.

Bango la kuwatetea wanablogu ya Free Zone9. Picha zimetumika kwa ruhusa.

Ungana na wanablogu wa Global Voices kwa ajili ya zoezi la kutwiti litakalofanyika duniani kote, katika lugha mbalimbali, kuwatetea wanablogu na waandishi kumi wanaokabiliwa na mashitaka ya ugaidi nchini Ethiopia.

Jumuiya ya Global Voices na mtandao wa washirika wake wanadai haki kwa watu hawa, wote waliofanya kazi kwa bidii kupanua uwanja wa maoni ya kijamii na kisiasa nchini Ethiopia kupitia blogu na uandishi wa habari. Tunaamini kukamatwa kwao ni uvunjaji wa haki za kimataifa za kujieleza, na kwamba mashitaka yaliyofunguliwa dhidi yao si halali. Unaweza kujifunza kujifunza zaidi kuhusu hadithi yao na kampeni ya kuwatoa kwenye Zone9 Blogu ya Kufuatilia Shauri hilo.

Shauri la wanablogu hao limeanza mnamo Agosti 4, 2014. Mpaka wakati huo, na hata zaidi, watahitaji kuungwa mkono kadri inavyowezekana. Kwa hiyo Alhamisi hii, sisi kama jumuiya ya wanablogu, waandishi, wanaharakati na wataalam wa uandishi wa kiraia walioenea duniani kote watashiriki ujumbe huu kwenda duniani kote, ku-twiti katika lugha za asili kwa viongozi wa mitaa, serikali, maafisa wa kidiplomasia na hata vyombo vikuu vya habari ili kuwafanya wafahamu kinachoendelea. .

Six of the detained bloggers in Addis Ababa. Photo used with permission.

Wanablogu sita waliokamatwa jijini Addis Ababa. Picha imetumiwa kwa ruhusa.

#FreeZone9Bloggers: Zoezi la kuwtiti Kushinikiza kuachiliwa kwa wanablogu wa ki-Ethiopia 

Tarehe: Alhamisi, Julai 31, 2014

Muda: Saa 4 asubuhi – 8 mchana — bila kujali unaishi wapi!

Alama habari: #FreeZone9Bloggers

Waandaaji: Nwachukwu Egbunike (@feathersproject), Ndesanjo Macha (@ndesanjo), Ellery Roberts Biddle (@ellerybiddle)

Unahitaji kuungana nasi Alhamisi hii? Au kusaidia kusambaza ujumbe? Ongeza jina na anuani yako ya Twita kwenye ukurasa wa mpango wa familia ya GV.

Mifano ya twiti:

    • @Zone9ers deserve a fair trial under international standards #FreeZone9Bloggers http://bit.ly

      @Zone9ers wanastahili shauri la haki linaloheshimu viwango vya kimataifa

      /1g65ijg 

    • Free the @Zone9ers… because blogging is not a crime! #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g65ijg

Waachieni @Zone9ers…kwa sababu kublogu si jinai!

    • “We blog because we care” #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g65ijg 

“Tunablogu kwa sababu tunajali”

    • Blogger arrests in #Ethiopia are a violation of the African Charter on Human and Peoples’ Rights #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/QlzRuG

      Kukamatwa kwa Wanablogu nchini Ethiopia ni ukiukwaji wa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu

    • Blogger arrests in #Ethiopia violate the International Covenant on Civil and Political Rights #FreeZone9Bloggers http://bit.ly/1g1MUNM

Kukamatwa kwa Wanablogu nchini Ethiopia ni ukiukwaji wa Makubaliano ya Kimataifa ya Haki na kiraia na kisiasa

Twiti mpaka vidole vyako viume na dai haki kwa wanablogu wa Zone9!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.