- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Alama ya Utambulisho wa Kompyuta ya Serikali ya Urusi Yakamatwa Ikihariri Makala ya Wikipedia ya Ndege ya MH17

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Ujerumani, Ukraine, Urusi, Habari za Hivi Punde, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala, Vita na Migogoro, RuNet Echo

Alama kadhaa za utambulisho wa kompyuta (IP address) ndani ya serikali ya Urusi zimeendelea kufanya kazi kazi kwenye kamusi elezo ya Wikipedia, ambapo kompyuta ya Shirika la Upelelezi la Urusi, FSO, ilihariri makala ya Kijerumani [1] kuhusu Ndege ya Shirika la Ndege la Malaysia MH17, ikibadili neno “wanaotaka kujitenga” kuwa “waasi.” [2] Teknolojia ya Twita ya @RuGovEdits [3], ambayo bila kuongozwa kufuatilia uhariri wowote unaofanywa kwenye kurasa za Wikipedia kupitia alama za utambulisho wa kompyuta za serikali ya Urusi, ilibaini majaribio saba tofauti [4] yaliyofanywa na kompyuta za “mashushushu” wa FSO asubuhi hii kuhakikisha kuwa neno “waasi” linabaki kwenye kumbukumbu. JItihada hizo zilikwama. Wahariri wa Kamusi Elezo ya Wikipedia kwa Kijerumani walirudisha maandishi ya awali yaliyokuwepo kwenye makala hiyo, kila mara.

Uhariri wa Kamusi elezo ya Wikipedia Kijerumani kuhusu MH17 kama unavyoletwa kwako na serikali ya Urusi.