Ajentina Yaichapa Uholanzi, Kukutana na Ujerumani Kwenye Fainali za Kombe la Dunia

LaPampa

La Pampa Ikiishangilia timu ya taifa ya Ajentina. Picha ya mtandao wa Flickr kutoka Wizara ya Taifa ya Utamaduni (CC BY-SA 2.0).

Mara ya mwisho kwa Ajentina kufika kwenye hatua ya fainali za Kombe la Dunia ilikuwa mwaka 1990, mashindano yalipofanyika nchini Italia na Ujerumani Magharibi ilitwaa kombe hilo. 

Baada ya kushinda dhidi ya Uholanzi kwa mikwaju ya penati 4-2 mnamo Julai 9, Ajentina inasonga mbele kufikia fainali kwa mara nyingine ikipambana na Ujerumani siku ya Jumapili, Julai 13 katika uwanja wa  Estádio Jornalista Mário Filho,ukifahamika zaidi kama Maracanã.

Blogu ya Esteban imeandika muhtasari wa mchezo huo kama ifuatavyo:

Un partido con historia de finales se avecina, con Alemania demoledora en el 1-7 ante los dueños de casa, en que a Brasil le faltó el alma que hoy a argentinos y holandeses les sobró.

Mchezo kati ya mataifa yaliyowahi kufika fainali mara nyingi unakaribia, wakati Ujerumani ikiicharaza Brazili kwa mabao 7-1 , na kuifanya Brazil ambayo ni mwenyeji wa mashindano hayo kukosa moyo ambao wa-Ajentina na Wadachi walikuwa nao kwa ziada.

Maeneo mengi maarufu ya Ajentina yaligeuzwa kuwa maeneo ya sherehe, na katika hali ya kushangaza, wa-Ajentina waliokuwa kwenye ufukwe wa Copacabana nchini Brazili walisherehekea pia:

Sherehe ya Ajentina kwenye ufukwe wa Copacabana kupitia @JornalOGlobo http://t.co/VbEnEFeqPB

Kwenye jiji la Buenos Aires, sehemu ya kukutania ilikuwa Obelisk, ambapo mashabiki walikuwa na mkesha:

ObeliscoBuenosAires

Picha ya kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Juan Pablo Paradelo.

Katika jiji la Rosario, walikozaliwa Lionel Messi, Ángel di María na Maxi Rodríguez, wachezaji watatu nyota wa kikosi cha Ajentina, wakazi walisherehekea kama ifuatavyo:

Rosario

Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa Rosario3.

Na hivi ndivyo kila mmoja alivyosherehekea huko Villaguay, kwenye jimbo la Entre Ríos:

Raota

Picha kutoka kwenye ukurasa wa Facebook wa José Luis Raota.

Kulikuwa na alama habari kadhaa zilizokuwa zikitumika kwenye mtandao wa Twita baada ya ushindi huo, kama vile #ArgentinaALaFinal (Ajentina yafika fainali), #EstamosEnLaFinal (Tumetinga fainali), #AlaFinal  (Fainali hatimaye) and #SiElDomingoGanamos (Kama tutashinda Jumapili):

#IfWeWinOnSunday [Kama tutashinda Jumapili] Nchi itafanya sherehe tena!

#IfWeWinOnSunday [Kama tutashinda Jumapili] Nitaacha kukosa shule, nimekuwa mtoro kwa siku kadhaa

Twiti iliyokuwa na matumaini:

#IfWeWinOnSunday [Kama tutashinda Jumapili] acheni kutumia neno ‘kama’ kwa sababu TUTASHINDA JUMAPILI

Wa-Ajentina wanataka kulipiza kisasi, na sasa wanahitaji tu kusubiri mpaka Jumapili:

Ujerumani, tazameni video zenu, madesa, lakini mnajua nini? tuna kazi ambayo inahitaji kukamilika kati yenu na sisi!

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.