Hata kabla ya timu ya taifa hilo kuichapa Uholanzi kusonga mbele kwenye fainali za Kombe la Dunia, Ajentina ilikuwa inasherehekea. Siku ya Julai 9 ni Siku ya Uhuru wa nchi hiyo, na ilikuwa ni siku moja kabla ya wapinzani wake wa asili Brazil hajatolewa nje ya mashindano baada ya kushishiwa kipigo cha fedheha cha mabao 7-1 na Ujerumani.
Furaha ilikuwa kubwa huko Tucumán, jiji lilikuwa msitari wa mbele kwa uhuru wa Ajentina na lilikuwa shahidi wa matukio ya mwaka 1816. Pale, bendi iitwayo Alto Peru Mounted Fanfare Band ilipiga wimbo inaoitwa “Brasil, decime qué se siente” (wenye maana ya, vipi hapo, Brazil!) ambao umekuwa maarufu sana kwenye Mashindano haya ya Kombe la Dunia.
Mashairi, yalikuwa na mahadhi ya ‘Bad Moon Rising’, unaokumbusha ushindi wa Ajentina dhidi ya Brazil kwenye fainali za Kombe la Dunia mwaka 1990 nchini Italia. Mchezo huo uliodumu bila magoli mpaka dakika ya mwisho ambapo Diego Maradona alimpasia mpira Claudio Caniggia, aliyeweza kuupachika wavuni na kumzidi maarifa mlinda mlango wa Brazili Taffarel. Ajentina ilifungwa na Ujerumani Magharibi katika fainali:
Brasil decime qué se siente tener en casa a tu papá / te juro que aunque pasen los años nunca lo vamos a olvidar / que el Diego los gambeteó, el Cani los vacunó / están llorando desde Italia hasta hoy// A Messi lo van a ver la copa nos va a traer// Maradona es más grande que Pelé.
Brazili, niambie unavyojisikia kumpokea baba yenu / Ninaapa kwamba hata kama muda utapita sitasahau / kwamba Diego [Maradona] aliwapita walinzi wako na [Claudio Caniggia] Cani akautia mpira kimiani / mmekuwa mkilia tangu enzi za Italia / mtamwona [Lionel] Messi akituletea kombe / Maradona ni mkali kuliko Pelé.
Habari na video ya bendi ya jeshi kupiga wimbo huo zilisambaa haraka sana kwenye mtandao wa Twita. Blogu yaAcordes 21 ilichapisha mpangilio wa sauti za wimbo huo kwa ajili ya kumsaidia yeyote anayependa kuuimba.
Mashabiki nyuma ya wimbo ni Ignacio Harraca na Patricio Scordo. Harraca alilieleza Gazeti la Ajentina Clarín kwamba baada ya kuthibitisha kwamba walikuwa wamekata tiketi kwa ajili ya kushuhudia mpambano huo wa Ajentina, yeye na rafiki zake walitaka kufanya jambo tofauti kusherehekea. Walipomaliza mashairi hayo, waliyasambaza kwenye mitandao ya kijamii na kwa njia ya makaratasi. Waliuimba wimbo huo mbele ya hoteli waliyofikia timu yao usiku wa kuamkia mpambano wa Bosnia:
Repartimos los folletos, y cuando se hizo un poco de silencio empezamos a cantarla. Al rato estaban todos prendidos y fueron como 40 minutos que se escuchó casi sin parar
Tulisambaza vipeperushi, na palipokuwa na ukimya kidogo tukaamua kuwanza kuimba. Baadae kidogo, kila mmoja akawa ameufahamu na kama kwa dakika 40 hivi wimbo uliimbwa kwa mfululizo.
Ajentina inacheza na Ujerumani kwenye fainali za Kombe la Dunia Jumapili, Julai 13.