Erik anatushirikisha taarifa 5 kuhusu mwenendo wa teknolojia barani Afrika:
Nimeendelea kutamani kuandika makala za blogu kuhusu taarifa hizi moja baada ya nyingine, nyingi zikihusu Afrika, lakini inaonekana sitaweza. Badala yake, nitaweka kiungo cha kila moja wapo, inayoonekana, na maneno machache ya kwa nini ni muhimu kuzisoma.
1. Taarifa ya Akamai kuhusu “Hali ya Mtandnao wa Intaneti” ya mwaka 2013.[Pakua [download] Taarifa ya Akamai, PDF]
Ina taarifa nzuri kuhusiana matumizi ya intaneti duniani, pamoja na mwenendo wake. Katika bara la Afrika, hata kama kuna maendeleo zaidi nchini Kenya, wote tunaona maendeleo pia yanayoonekana katika nchi za Afrika Kusini, Misri na Moroko. Hata hivyo, kuna mchoro wa Ericsson kuhusu matumizi ya mtandao wa si-waya.