- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Simulizi la Kusikitisha la Ibrahim na Djouma wa Jamhuri ya Afrika ya Kati

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Kameruni, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Mahusiano ya Kimataifa, Mwitikio wa Kihisani, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Vijana, Vita na Migogoro, Wakimbizi
Ibrahim and Amadou - screen capture of UNHCR video on YouTube [1]

Ibrahim na Amadou – picha iliyopigwa kwenye video ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kushughulikia wakimbizi (UNHCR) kwneye mtandao wa YouTube

Djouma na Amadou Moussa ni wazazi wa Ibrahim. Djouma na Ibahim ni wahanga wa shambulizi la kikatili lililofanywa na  wanamgambo waaasi, tukio lililokatisha maisha ya ndugu watano wa damu katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, karibu na mpaka wa Kameruni. Wanamgambo hao walikuja wakati  Amadou Moussa akiwa mbali na nyumbani kwake. Djouma, 30, anakumbuka tukio hilo baya [2]

Walinikuta nikiwa na wanangu nyumbani kwangu; waliwakusanya watoto wote wadogo na kuwachinja kwa panga. Waliua watu sita, ikiwa ni pamoja na watoto mbele yangu [..] Ibrahim alikuwa kati ya watoto sita waliowachukua. Walimkata na panga, wakadhani amefariki.

Kama inavyoonekana kwenye video hii [1], Ibrahim ana kovu kubwa kichwani kwake lililosababishwa na panga. Hata hivyo Ibrahim alipona, pamoja na tukio hilo baya. Hadithi ya Ibrahim ni mfano wa madhila ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati. Wakimbizi 20,000 wamevuka mpaka tangu kuanza kwa vita. Ombi maalum limetumwa kwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani John Kerry kumkumbusha [3] kuchukua “hatua stahiki za kuhakikisha  kwamba mikakati ya kurejesha amani inatengewa fedha kwa mwaka wa 2015.”