- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Sababu za Kuishangilia Kodivaa kwenye Kombe la Dunia

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Amerika Kusini, Brazil, Colombia, Cote d'Ivoire, Peru, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia
CostadeMarfil

Timu ya Taifa ya Kodivaa wakati wa Mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA, mwaka 2010, nchini Afrika Kusini. Picha ni ya mtumiaji wa mtandao wa Flickr, Merah Chhaya [1]. CC BY 2.0.

Kwenye tovuti ya LaMula.pe, Juan Carlos Urtecho anaeleza sababu zake [2] za kuishangilia Kodivaa kwenye mpambano wa Kombe la Dunia kati ya nchi hiyo na Kolombia siku ya Alhamisi, Juni 19:

Desde que les ganaron a Japón en su debut, los marfileños se han vuelto mis preferidos en este mundial. […] Uno escoge a sus engreídos de la manera más simple. Costa de Marfil, ubicado en la costa occidental de África, con un PBI de 19 mil millones de euros y un per cápita de 967 euros es el tercer país más pobre de los que están en el mundial después de Honduras y Bosnia. La economía de Japón (PBI de 5 billones de euros y 30 mil per cápita) es la segunda detrás de Estados Unidos. Costa de Marfil es un país que intenta recuperarse de una sangrienta guerra civil que dejó a decenas de miles de muertos y cientos de miles de desplazados entre el 2002 y el 2007. Japón, es… bueno, Japón.

Tangu wakati waliposhinda Japan katika mechi yao ya awali, hawa jamaa [Wakodivaa] wamekuwa timu yangu pendwa kwenye mashindano haya ya Kombe la Dunia […] Unachagua mayai viza kwa njia rahisi. Kodivaa, nchi iliyoko Afrika Magharibi yenye Pato la Nchi la Euro milioni 19 na wastani wa Euro 967 kwa kila Mkodivaa, ni nchi maskini zaidi kati ya nchi zinazoshiriki kwenye mashindano hayo, baada ya Honduras na Bosnia. Uchumi wa Japani (Pato la Taifa la Euro bilioni 5 na wastani wa Euro milioni 30 kwa kila Mjapani) ni wa pili baada ya Marekani. Kodivaa ni nchi inayojikakamua kupata nafuu baada ya vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe vilivyoua makumi ya maelfu ya watu na kuwahamisha malaki ya watu kutoka kwenye makazi yao kati ya mwaka 2002 na mwaka 2007. Japan, ni…aha, ni Japan.