- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ni Rasmi Sasa, ‘Shoga’ wa Kwanza Kuteuliwa Kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Nchini Puerto Rico

Mada za Habari: Amerika Kusini, Nchi za Caribiani, Puerto Rico (Marekani), Habari Njema, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Haki za Mashoga, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia
Maite Oronoz durante el proceso de confirmación en el Senado de Puerto Rico. Imagen tomada de video. [1]

Maite Oronoz wakati wa zoezi la kuthibitishwa kwenye baraza la seneti la Puerto Rico. Picha imepigwa kwenye video iliyowekwa na Baraza la Seneti.

[Viungo vyote vinaelekeza kwenye kurasa za lugha ya Kihispania, isipokuwa ikionyeshwa vinginevyo.]

Mnamo Jumatatu, Juni 23, 2014, Baraza la Seneti la Puerto Rico lilimthibitisha mwanasheria Maite Oronoz Rodríguez [2] [en] kuwa Jaji wa Mahakama Kuu nchini humo. Uteuzi huo wa kihistoria unakuwa wa kwanza kwa mtu aliyejitangaza kuwa msagaji kuteuliwa kuitumikia mahakama kuu kabisa nchini humo. Oronoz Rodríguez, ambaye anakuwa mwanamke wa tano kuitumikia Mahakama Kuu, alitoa shukrani zake kupitia tamko la maandishi [3] [en]:

Ninayo furaha kwamba mchakato wa kidemokrasia umesababisha niteuliwe. Ninajivunia kuendelea kuitumikia nchi yangu, wakati huu kwenye Mahakama Kuu. Kujitolea kwangu kwa nchi yangu na kwa katiba ya Puerto Rico kutaendelea kuwa imara. Kupitia kwangu, watu wa Puerto Rico watapata jaji mwaminifu wa mtenda haki, mtiifu kwa katiba ya nchi. Ninamshukuru Gavana na Baraza la Seneta kwa fursa ya kuthibitisha kujitolea kwangu.

Kura ya kumthibitisha Oronoz Rodríguez ilikabiliwa na upinzani mkali, kura 16 zikimkubali na 10 zikimkataa [Oronoz aliteuliwa na gavana wa Puerto Rico, Alejandro García Padilla, wa chama cha Kidemokrasia cha Partido Popular Democrático]. Katika kura zilizomkataa Oronoz Rodríguez ilikuwemo ya Seneta pekee wa kike, wa chama cha Puerto Rican Independence Party, María de Lourdes Santiago. Santiago alieleza [4]kuwa uamuzi wake ulizingatia uhusika wa Oronoz Rodríguez katika kashfa za siku za nyuma, ambapo inadaiwa akiwa mkurugenzi wa Idara ya Sheria ya Manispaa ya San Juan alitetea uamuzi wa Meya wa kuruhusu kukaguliwa kwa kila mtu ambaye angehudhuria Sherehe za Mtaa wa San Sebastian. Kukaguliwa kulithibitishwa na mahakama ya sheria kuwa kinyume na katiba.

Mchakato wa kuthibitishwa haukupia hivi hivi. Baada ya kura iliyomthibitisha Oronoz Rodríguez kuwa Jaji wa Mahakama Kuu, baadhi ya maseneta waliomba [5] kuhesabiwa upya kwa kura. Amárilis Pagán (@AmarilisPagan [6]), mwanasheria wa kutetea haki za Mashoga (LGBT), alionyesha kusikitishwa kwake na mchakato huo:

Kama pasingekuwa na hofu na chuki dhidi ya mashoga mjini humu, tusingekuwa na zengwe hili la kuthibitishwa kwa Oronoz. Ni mchosho wa taifa. 

Mwanaharakati wa Haki za Mashoga Pedro Julio Serrano alikisifu [8] kitendo cha Oronoz Rodríguez wakati wa mchakato wa kuthibitishwa: 

Maite se presentó sin miedo – con todas sus identidades a flor de piel y ante la vista del País. Su nombramiento merecía esa misma valentía. Lo tuvo, a final de cuentas, pero de manera atropellada. Hay que ir de frente, sin miedo, de cara al sol, con respeto y dignidad. Como merecemos las personas LGBTT, como merecemos tod@s l@s seres human@s.

Maite alijieleza bila hofu – akijitambulisha kikamilifu kama mpenda nchi. Uteuzi wake [kama Jaji] unathibitisha hili. Ilitokea, mwisho wa siku, lakini kwa namna ya kushangaza. Lazima tuendelee mbele, bila woga, tukilitazama jua, kwa heshima na hadhi inayostahili. Kama watu wapendao mapenzi ya jinsia moja wanavyostahili. Kama binadamu wote wanavyostahili.

Jaji mpya alipongezwa na wabunge wa nchi hiyo, Luis Gutiérrez na Nydia Velázquez kupitia mtandao wa twita:

Ni siku kubwa kwa usawa wa kimapenzi na haki kwa mashoga. Ninampongeza gavana kwa kumteua Maite Oronoz Rodriguez kuwa jaji

Si tu kuwa Maite Oronoz atakuwa jaji bora lakini uteuzi wake kuwa jaji wa Mahakama Kuu ni hatua moja mbele kwa haki za kiraia

Katika safu ya jarida la mtandaoni 80 grados, mwanaharakati Yoryie Irizarry (@CyborgYoryie [12]) alilitazama tukio hili la kihistoria kama matunda ya mapambano ya muda mrefu ya kudai usawa [13] yaliyoongozwa na jumuiya ya mashoga na wasagaji:

A diferencia de lo que piensan nuestras aliadas y aliados, yo he decidido pensar que ese momento histórico no nos viene cortesía del gobernador Alejandro García Padilla. Este momento histórico nos lo hemos ganado en las calles, en las legislaturas, en nuestras comunidades y empleos, educando, haciéndonos visibles, deponiendo, escribiendo, firmando cartas, debatiendo y trabajando.

Kinyume na kile washirika wetu wanavyodhani, nimeamua kufikiri kwamba tukio hili la kihistoria halijatokea kwa nguvu za Gavana Alejandro García Padilla. Tumeshuhudia tukio hili mitaani, bungeni, na kwenye jamii zetu na kwenye shemu zetu za kazi, kuelimisha, kujitangaza, kushuhudia, kuandika, kusaini barua, kupambana na tunaona kazi inaendelea.

Mjadala wa umma ulionzishwa na uteuzi wa Oronoz Rodríguez unabainisha mwamko endelevu wa hali ya kimapenzi hata kwa watu maarufu, kufikia mahali masuala ya msingi, kama uwezo na uelewa wake, vitafutika kwa sababu tu ya hali yake ya kimapenzi. Katika makala yake kwa jarida la mtandaoni la El Post Antillano, Jaime Pieras Castañer alielezea [14]tatizo hilo:

Cuando se discutía el nombramiento en los medios se enfatizaba demasiado en la orientación social de la nominada. Aparentemente, hubiese estado bien si no fuese sincera sobre su orientación sexual, pero lo dijo. Thomas Rivera Schatz, ex presidente del Senado, expresó en un apasionado discurso […] en el Senado que ella era la que había traído a la atención que era lesbiana. Bah, como si eso tuviese que ver con sus clasificaciones o con las consideraciones que deben de ser parte de cualquier deliberación sobre los dotes o el talento de Oronoz.

Vyombo vya habari vimeupa uteuzi huu sura ya mwelekeo wa kijinsia wa mtauliwa. Kwa hakika, ingekuwa vyema kama asingekuwa wazi kuhusu hali yake ya kimapenzi, lakini ndio hivyo, alishajitangaza. Thomas Rivera Schatz, rais wa zamani wa Seneti, alisema kwenye hotuba yake kali […] kwneye Seneta kwamba [Oronoz Rodríguez] mwenyewe ndiye aliyelileta suala la usagaji wake hadharani. Utafikiri hali yake ya kimapenzi ina maana yoyote kwa sifa zake au iwe sababu yoyote ambayo yapaswa kuwa sehemu ya mjadala wa vipaji na uwezo wa Oronoz.

Érika Fontánez Torres, mwanasheria, Profesa wa Sheria na mhariri wa jarida la mtandaoni Derecho al Derecho, anatoa maoni ya kusisimua kwenye podikasti [15] ya jarida hilo (kwenye dakika ya 11:20):

Hay alguna gente que a raíz de toda esta discusión ha dicho “no, es que no es importante, no es relevante que ella sea lesbiana o no” y, bueno, lo primero que tendríamos que decir, “sí, que sí que lo es”, […] sí que las subjetividades son importantes en el Tribunal, sí que añaden a la mesa, sí que la diversidad es importante a la hora de la deliberación de los jueces […], y si esa persona tiene, como en el caso de Maite Oronoz, una experiencia de vida desde esa ubicación, eso me parece extraordinario.

Kuna baadhi ya watu waliojibu mjadala huu kwa kusema, “Hapana, si tatizo, haina maana awe ni msagaji au sio,” lakini sawa, jambo la kwanza tunalopaswa kuwa tunalisema ni “Ndio, ndo, ni muhimu”…ndio, maamuzi binafsi ni muhimu kwenye mahakama, ndio, yanaleta jambo fulani kwenye kazi zake za kila siku, ndio, tofauti ni muhimu majaji wnaapotekeleza kazi zao […], na kama mtu binafsi, kama Maite Oronoz, ana uzoefu wa kimaisha kwa mtazamo huo, ningeweza kusema kwamba kuwa hilo ni suala kubwa isivyo kawaida.