- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mapigano Dhidi ya Waislamu Yaendelea Nchini Sri Lanka

Mada za Habari: Asia ya Kusini, Sri Lanka, Haki za Binadamu, Majanga, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vita na Migogoro

Yametimu majuma mawili tangu ghasia dhidi ya Waislamu [1] kwenye majiji ya pwani nchini Sri Lank- Aluthgama na Beruwala. Ingawa hali imetulia baada ya kulaaniwa sana [2] kila sehemu, bado ghasia hizo dhidi ya Waislamu zinaendelea [3] katika maeneo tofauti ya Sri Lanka.

Mwanablogu Abdul Khaleq [4] anatwiti kuhusu tukio moja huko Ratmalana [5] sehemu ya wilaya ya Colombo:

Msikiti ulioko barabara ya Ratmalana Borupona umechomwa moto saa 7 usiku. Moto ulioanza mapema ulizimwa.

Mwanablogu D. B. S. Jeyaraj [8] ana habari zaidi kuhusu jaribio lililoshindwa la kushambulia msikiti wa Thalayan Bawa Jumma uliopo kwenye barabara ya Borupane mjini Ratmalana masaa ya asubuhi Jumapili iliyopita, tarehe 29 Juni, 2014.