Yametimu majuma mawili tangu ghasia dhidi ya Waislamu kwenye majiji ya pwani nchini Sri Lank- Aluthgama na Beruwala. Ingawa hali imetulia baada ya kulaaniwa sana kila sehemu, bado ghasia hizo dhidi ya Waislamu zinaendelea katika maeneo tofauti ya Sri Lanka.
Mwanablogu Abdul Khaleq anatwiti kuhusu tukio moja huko Ratmalana sehemu ya wilaya ya Colombo:
Ratmalana Borupona Rd mosque set on fire 1am. Flames spotted early and put out. Min Fowzie here #StayStrongSrilanka pic.twitter.com/Vys16T51vn
— abdulkhaleq (@HalikAzeez) June 29, 2014
Msikiti ulioko barabara ya Ratmalana Borupona umechomwa moto saa 7 usiku. Moto ulioanza mapema ulizimwa.
Mwanablogu D. B. S. Jeyaraj ana habari zaidi kuhusu jaribio lililoshindwa la kushambulia msikiti wa Thalayan Bawa Jumma uliopo kwenye barabara ya Borupane mjini Ratmalana masaa ya asubuhi Jumapili iliyopita, tarehe 29 Juni, 2014.