Kijana Huyu Mwenye Asili ya Zambia Awa Mwanafunzi wa Kwanza Kuwa Mtalaam wa Kutegemewa na Microsoft

Kijana mwenye asili ya Zambia, lakini anayeishi Uingereza mwenye miaka 15 Samkeliso Kimbinyi anatengeneza zana za kupiga soga mtandaoni kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano na hivyo kuwa mmoja wa wataalam wadogo zaidi waliobobea na wanaotumiwa na kampuni ya Microsoft barani Ulaya.

Kijana huyo mdogo, anayefahamika zaidi kwa jina la Sam, mwanafunzi wa darasa la 10 (sawa na sekondari ya juu) kwenye Chuo cha Teknolojia (UTC) huko Reading, mji ulioko nje kidogo ya London. Kwa sasa ni Mtaalam Anayekubalika na Microsoft na ana vyeti vya Ufundi vya Microsoft (MTA) katika maeneo saba ikiwa ni pamoja na Mafunzo ya Msingi za Zana, Mafunzo ya Uundaji wa Program za Windows na yale ya utengenezaji wa mifumo (OS).  

Kimbinyi pia ameunda zana tumizi (app) iitwayo Lite kwa simu zenye zana ya Windows na mpaka sasa ameendelea kupata maoni chanya kwa kazi hiyo.

Sam Kimbinyi's Twitter profile photo.

Picha ya Sam Kimbinyi imechukuliwa kwenye wasifu wake wa Twita.

Global Voices Online ilikutana naye kupitia barua pepe na kutaka kujua kutoka kwake moja kwa moja kuhusu mafanikio yake:

Mwezi Machi mwaka huu, nilikuwa na fursa ya kukutana na wafanyakazi wa Ofisi ya Microsoft pale Seattle, ambao walikuwa Uingereza kwa siku moja kama sehemu ya ziara yao ya Ulaya wakizungumza na wateja wao wanaopata mafunzo kwenye Chuo chao cha Taknolojia na Mawasiliano cha Microsoft. Walikuwa ni wale wa timu ya Mafunzo -Mkurugenzi Mwandamizi Tim Sneath, Mkurugenzi wa Program za Mafunzo Keith Loeber na Mkurugenzi wa Maudhui Briana Roberts.

Mnamo Mwezi Mei 26th 2014 nilichapisha toleo la kwanza la zana ya App—Lite—on ya simu zenye mfumo wa Windows. Nilipata wazo la kutengeneza zana tumizi hii baada ya kutumia masaa mengi nikitafuta zana ambayo ingenisaidia kufanya kazi zangu bila kujaa matangazo mengi. Hatimaye, baada ya kushindwa kupata nilichotaka, niliamua kutengeneza yangu mwenyewe. Siku nane baadae na baada ya kukosolewa sana na Jumuiya ya Reddit ya Simu za mfumo wa Wondows, nilipata habari njema za mipakuo [downloads] ipatayo 300 na wengine waliipa alama za juu kwamba inafaa. Baada ya muda, ikawa kwenye kundi la “Mpya na Inapata Umaarufu” kwenye sehemu ya mauzo ya bidhaa mtandaoni.

Mbeleni ninatarajia kutoa zana tumizi zaidi na kuendelea kujifunza zaidi fani ya Sayansi ya Kompyuta chuoni.

Kwenye kijarida cha chuoni kwake, Kimbinyi alinukuliwa alisema:

Mafunzo Microsoft yanajaribu kutumia kile tunachokisoma darasani, lakini yamenipa uelewa mpana wa ujenzi wa programu na namna tasnia hiyo ilivyo pana. Ufahamu wangu mpya ulikuwa wa muhimu sana tulipotengeneza zana tumizi wakati wa mradi wa mwajiri wa Microsoft; tukaishia kuunda zana [app] bora zaidi.

Microsoft ilimpongeza Kimbinyi kwenye twiti hii:

Hongera sana kwa Samkeliso Kimbinyi, miaka 15, mwanafunzi wa kwanza kupata sifa za kituo cha mafunzo cha Microsoft katika utengenezaji wa zana

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.