Kikundi cha Kitalibani Chasema Shambulio la Uwanja wa Ndege wa Karachi Lililoua Watu 24 Lilikuwa ‘Kisasi’

Photo tweeted by Twitter user @ahsannagi #KarachiAirport. Pic by a friend stuck there - M. Qasim. #Rangers can be seen.

Picha ilikuwa kwenye twiti ya mtumiaji wa Twita @ahsannagi #KarachiAirport. “Picha iliyotumwa na rafiki yangu aliyeko uwanjani – M. Qasim. #Wanajeshi wanaweza kuonekana kwenye Uwanja wa Ndege”

Hii ni habari inayoendelea kuandikwa. Habari za hivi karibuni ziliingia saa 12:22 GMT, Tarehe 9 Juni:

Kikundi cha kigaidi cha Tehreek-i-Taliban Pakistan (TTP)  kimedai kuhusika na tukio hilo , kikisema kuwailikuwa ni kulipiza kisasi kufuatia shambulio la anga lililofanywa na jeshi la Pakistani kwenye mpaka wa nchi hiyo na Afghanistani.

Gazeti la kila siku linaloongoza la Pakistani, Dawn linasema kuwa operesheni ya kijeshi ilianzishwa upya kwenye uwanja wa ndege wa Karach, kufuatia  majibizano ya risasi, yaliyoanza masaa kadhaa baada ya jeshi kusema kwamba lilikuwa limefanikiwa kurejesha hali ya usalama kwenye uwanja huo wa ndege wenye shughuli nyingi zaidi nchini humo, kufuatia uvamizi wa wanamgambo wa kigaidi kuteka uwanja huo kwa masaa sita na kupoteza maisha ya watu wapatao 24. 

Kutoka kwenye gazeti hilo la Dawn: “Tumeanza operesheni mpya na tumeita vikosi vipya,” alisema Sibtain Rizvi, msemaji wa kikosi cha jeshi cha Karachi.

Kabla ya saa 11 alfajiri, kwa saa za Pakistani, jeshi lilitoa taarifa kwamba wavamizi wote 10 walikuwa wameuawa. Wanasemekana waliingia uwanjani humo kwa kutumia vitambulisho bandia vya wanausalama wa uwanja huo wa ndege  wakiwa na , silaha kali na mabomu ya kutupa kwa mkono.

Karachi Airport employees being escorted out of Jinnah International Airport. Photo tweeted by Dawn_com

Wafanyakazi wa Uwanja wa Karachi wakisaidiwa kutoka kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jinnah. Picha ilitwitiwa na @Dawn_com


Mtu mmoja alijitoa mhanga wakati wa shambulizi hilo. Watu 14 waliokuwa wafanyakazi wa uwanja huo, wengine wakiwa wafanyakazi wa shirika la ndege la taifa la Pakistani na vikosi vya usalama vile vile walipoteza maisha. Wasafiri wote waliokuwa wamekwama kwenye ndege wakati mapambano hayo yakiendelea waliokolewa na kupelekwa kwenye sehemu ya kukaa abiria baada ya shambulio hilo kumalizwa. Wanamgambo hao waliharibu ndege tatu ambazo hata hivyo hazikuwa na abiria ndani.

—————————————–

Sehemu ya zamani ya kupumzikia abiria katika uwanja wa ndege mkubwa zaidi nchini Pakistani – Uwnaja wa Ndege wa Kimataifa wa Jinnah ilikumbwa na shambulizi zito lililofanywa na wanamgambo wenye silaha usiku wa kuamkia Jumatatu. Wanamgambo wote wenye silaha wanasemekana kuingia kwenye sehemu hiyo ya uwanja iliyokuwa imetengewa kwa ajili ya watu maarufu na shughuli za ndege za Hajj, lakini kwa mujibu wa ramani ya uwanja huo, ndege zote huchangia njia moja ya kupaa au kutua.

Mtumiaji huyu wa Twita – Syed Saim Rizvi – alikuwa kwenye ndege ya Emirates iliyokuwa uwanjani humo wakati wa mapambano hayo:

Sina maneno ya kusema kwa ajili ya wafanyakazi wa Emirates, ambao wanajitahidi kuwatuliza abiria

Mlipuko wa kutisha!!! Sijui kinachoendelea mule ndani….milio ya risasi imeanza tena -humu kwenye ndege watu wako kwenye tahayaruki mno!

Awali alikuwa ametwiti:

Bado niko kwenye ndege -mfanyakazi wa emirates aliamuru mapema kwamba abiria washuke lakini kwa sasa imebidi tubaki kwenye ndege. Milipuko mikubwa inasikika

Hivi ndivyo shambulio lilivyofahamika:

Shughuli za kutua na kupaa kwa ndege zimesitishwa kwa muda kwenye uwanja wa ndege kimataifa wa Jinnah ulioko Karachi kufuatia hali ya kukosekana usalama. Tafadhali piga simu namba 114 kwa taarifa zaidi.

Uwanja wa ndege wa Karachi umetekwa na washambuliaji wa kigaidi wanaosemekana kuwa kati ya 15 -20. Hali ya hatari imetangazwa katika viwanja vyote vya ndege vya Pakistani

Picha ya rafiki yangu aliyekwama ndani ya ndege. Wanajeshi wanaweza kuonekana.

Makomandoo na magaidi wanajibizana kwa risasi wakati huu. Bado ninasikia kwa karibu. Idadi ya washambuliaji inasemekana kuwa kati ya 10 -15.

Approx 4-5 hand grenades used in the attack. Dark smoke visible from where planes were. #karachi— عادل (@aurAdil) June 8, 2014

Kadri ya mabomu ya kutupwa kwa mkono yapatayo manne hadi matano yametumiwa kwenye mashambulizi. Moshi mzito inaonekana nyuma palipokuwa na ndege

Katika hali hii ya kusikitisha, maombi yangu yaende kwa familia za wafanyakazi wa uwanja huu na wa mashirika ya ndege ambao mpaka sasa wamethibitika kupoteza maisha yao kwneye uwanja huu

Lililo muhimu zaidi, bado kuna abiria waliokwama kwenye ndege iliyokuwa kwenye njia ya kutua ndege.

Magaidi watatu wako ndani ya uwanja. Milio ya milipuko inasikika. Bila shaka kila mmoja yuko salama

Wakati washambuliaji na operesheni ikiendelea baadhi ya watu waliisifu anuani ya twita ya @AirportPakistan:

@AirportPakistanni mfano wa namna mamlaka zinapaswa kutumia mitandao ya kijamii wakati wa majanga ili kutoa habari na kurekebisha tetesi na uvumi.

Habari sahihi kwa wakati muafaka kuhusu ratiba za ndege na utaratibu wa kuelekeza ndege kutua kwingineko

Baadhi ya watu walifananisha shambulio hili kwneye uwanja wa ndege wa Karachi na lile la eneo la Mehran  lililotokea Karachi mwaka 2011.

Je, ni kwamba tunashuhudia tukio jingine la #MehranBase?

Katika shambulio lililopita la Mehran ilichukua siku mbili kurejesha hali ya usalama…na hili ni kubwa mara kumi ya eneo la Mehran…!!!

Wakati vyombo vya habari vikitangaza habari za operesheni maalumu ya kijeshi, baadhi ya watu walilalimika kuhusu kutokuwepo kwa usalama kwenye eneo la uwanja wa ndege.

Shambulizi la GHQ, Shambulizi la Mehran, SHambulio la PAF, Shambulio la uwanja wa ndege wa Khi, na sasa uwanja wa ndege wa Jinnah, ndugu zangu msiogope, tuna vyombo madhubuti kabisa vya usalama kuzidi vyote duniani

Kazi za ndani ya uwanja huo kwenye sehemu ya kupakua na kupakia mizigo nayo imeshambuliwa kama ilivyokuwa Mehran. Sehemu ya kutua na kupaa kwa ndege zimedhibitiwa…vyombo vya usalama vya Pakistani viko juu

Kwa hiyo kiongozi shupavu: “Nawaz Sharif amewaelekeza wanajeshi kuhakikisha usalama wa abiria wote kwneye uwanja wa ndege

Kwa bahati mbaya, kama ilivyo kawaida ya uandishi wa habari kadri zinavyotokea, kulikuwa na tarifa za kujichanganya kuhusu idadi hasa ya washambuliaji, pamoja na tetesi kuhusu ndege kulipuliwa au kutekwa, hapa unaweza kuona baadhi ya miitikio kutoka kwneye mtandao wa Twita dhidi ya taarifa za utatanishi zilizokuwa zinatangazwa:

Mtu si awaambie watangazaji a vyombo vikuu vya habari kwamba kanuni ya kwanza ya kutangaza habari ni kutokuonyesha uko upande gani? Wanachokifanya ni dalili kwamba hawajafuzu vyema

Vyombo vya habari LAZIMA vichukue hatua ya kurudi nyuma SASA. Hakuna haja ya kutangaza mbinu za kijeshi au kutoa habari za tetesi zisizo na ushahidi

Vyombo vya kijinga vya habari vinatoa taarifa za uongo kuhusu shambulio la uwanja wa Karachi. Ndege haijatekwa. Wamezidiwa sasa na Polisi

Vyombo vya habari vinaonyesha kwa kina kila kinachoendelea wakati huu kwa matangazo ya moja kwa moja. Je, havikupaswa kuficha baadhi ya taarifa?

Hapana ndege haijatekwa wala magaidi hawajaingia kwneye ndege yoyote isiyo na aibiria

Twiti hii ilitumwa wakati wanajeshi wa Pakistani walipoungana kwneye operesheni iliyokuwa inafanywa na wanajeshi wakishirikiana na vyombo vya usalama vya uwanja huo wa ndege. Waziri Kiongozi wa Sindh pia aliwasili kwenye eneo la tukio kukagua hali ya usalama.

Waziri Kiongozi Sindh ana makomandoo zaidi kuliko waliopo kwenye uwanja wa ndege wa Khi sasa hivi? Hiki ni kioja kwa serikali ya Sindh isiyokuwa na aibu!!!

Hii ni habari inayoendelea kuandikwa kadri habari zinavyoendelea kupatikana, kwa habari za hivi karibuni zaidi fuatilia@AirportPakistan, @AsimBajwaISPR

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.