Baada ya Waziri wa India Kusema ‘Wakati Mwingine Ubakaji Unakubalika’, Kampeni ya #MenAgainstRape Yavuma Nchini Pakistani

Photo Credit: Philipp Engelhorn

Picha mali ya: Philipp Engelhorn

Je, ni rahisi kulaani ubakaji unapotokea sehemu nyinginezo? Vipi ikiwa vitendo hivyo vitatokea nje ya mipaka ya nchi? Alama habari ya  #MenAgainstRape imeanza kuvuma kwa mara nyingine, wakati huu nchini Pakistani, habari zinadai kuwa baada ya  Babulal Gaur, waziri wa mambo ya ndani wa India, alitoa  matamshi haya kuhusu ubakaji, ‘wakati mwingine ni sahihi, wakati mwingine huwa ni makosa’.

Mamia ya vijana kutoka Pakistan walijiunga na kampeni ya kupinga ubakaji. Mtumiaji wa mtandao wa Twita wa Pakistani ambaye anuani yake ya twita baysharam ina maana ya ‘asiye na woga’ aliungana na wenzake kw akusema:

Mnamkumbuka binti wa miaka mitano aliyebakwa huko Lahore, mwaka jana? Mwanamme aliyembaka (huenda walikuwa wengi pia) bado wanatamba mitaani. Wako miongoni mwetu.

Wakati wa habari za ubakaji wa kimakundi jijini Delhi mwaka 2012 zilipovuma katika vyombo vya habari, mamia ya twiti zilitoka nchini Pakistani kulaani matukio hayo ya kifedhuli. Baadhi walizungumzia matatizo ya ubakaji nchini India wakati wengine waliyatazama matukio yanayoibukia katika maeneo mengine ya Asia Kusini. Zilikuwa ni habari mbaya za kutisha kiasi kwamba macho ya vyombo vya habari yalielekezwa eneo hilo kwa majuma kadhaa na mpaka leo habari zinazohusiana na ubakaji zinaendelea kushika kasi nchini India tangu wakati huo.
Mwanablogu wa Kihindi Krshna Prashant alizungumzia imani potofu kuhusu ubakaji kwenye andiko lake lililo kwenye mtindo wa kejeli:

Aliingia kwenye saa 5 usiku. Aliosha vyombo kimya, moyo wake ukidunda aliposikia hatua za mtu anayechechemea kumwendea. Machozi yalimlenga lenga wakati jamaa anaweka mikoni kiunoni mwake. Alisikia harifu ya pombe kwenye pumzi yake. Alimpapasa na nguo ya pallu aliyokuwa ameivaa, ikadondoka sakafuni. Tusifanye leo, alimwomba. Mgongo wake uliuma na kichwa chake kilikuwa kama kinakaribia kupasuka.

Alimshika nywele na kumvuta kuelekea kwenye chumba chake. Alihangaika kuiokota nguo yake wakati wakitembea. Mtoto wao aliwatazama kwa mshangao. Alimfungia mlango na kuchapa kibao. Alimwamuru kuwa kimya na kuvua nguo. Alifanya kama alivyoamriwa.
Unamaanisha nini unapsema mtoto wangu alimbaka mke wake. Hakuna kitu kama hicho.

Huu, ni mtazamo mwepesi na wenye nguvu dhidi ya unyanyasaji, hata hivyo ukitazama kwa makini kwenye twiti hizi utaona imani nyingi ambazo Prashant alizizungumzia.

Anayewaomba msamaha wabakaji (jina): Mtu yeyote anayewatetea wabakaji AU anayeona ubakaji kuwa ni jambo la mzaha.

Hapa ni baadhi ya mitazamo ya utetezi wa wazi wazi wa ubakaji Asia Kusini:

Wanavaa mavazi yenye ushawishi na kutamanisha watu na kuishia kubakwa. Huu si ubakaji, ni ngono ya ridhaa.

#TunaopingaUbakaji lakini kwanza tuma picha zako za uchi kwenye mtandao wa Whatsapp

Kila mbakaji lazima abakwe hadharani…na tuwaache wabaki hai…sasa uone watakavyofanya mambo ya ajabu duniani….

Wengine walitumia alama habari hiyo kupendekeza kuwa ukatili wa kimapenzi ndio uwe adhabu ya wabakaji:

Wakati pekee ninapojikuta naunga mkono ubakaji! #Tunapopinga ubakaji…kuwabaka wanaobaka ndio iwe adhabu yao!

Mnaonaje wazo la kukata sehemu zao za siri na kusaga kabisa viungo vyao!??
Wengine walikuwa na maoni yaliyopitiliza.

Kwa sababu tu hakusema HAPANA…. haimaanishi kuwa anasema NDIYO

Ubakaji ni ubakaji na haukubaliki kwa vyovyote. Ni kitendo cha kikatili sana na ni lazima kikomeshwe kwenye jamii yetu

Kila mwanaume lazima ashiriki kampeni hii

Hivi tangu lini nguo wanazovaa wanawake ziwe chanzo cha matatizo kwa kila mwanaume duniani humu?

Ubakaji ni kitendo cha aibu, kinaudhi na kiovu mno kw amtu kukifanya. Kuwa mtetezi wa wabakaji ni kitu cha ajabu

Kuwageuzia kibao wahanga wa ubakaji kuwa ndio wanaosababisha wabakwe ni sawa na kumlaumu aliyeuawa kwa kuuawa

Wakati wengi wanadhani kuwa hatua hii ya wanaume kusimama kidete kupambana na ubakaji ni hatua kubwa, wengine wanahoji ufanisi wa majadiliano ya kwenye mtandao wa Twita ukilinganisha na matukio halisi ya nje ya mtandao. Je, kampeni hii itabadili namna wahanga wa ubakaji wanavyoonekana katika jamii? Je, itakomesha ubakaji kutotokea tena? Je, itasababisha taasisi za kisheria kuchukua hatua? Haya ni baadhi ya maswali yanayoibuliwa. Iwe kwamba uko upande wa wenye wasiwasi na kampeni ya mtandaoni au una imani kubwa na kampeni hiyo, ya kupinga ubakaji ya #menagainstrape inatoa mwanga mdogokwneye akili za vijana wadogo kuhusu uelewa wao kuhusina na na ukatili wa kijinsia.. 

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.