Jinsi Mabadiliko ya Hali ya Hewa Yanavyowaathiri Wakaazi wa Vijiji Nchini Benin

Mbenin, Alain TOSSOUNON, alipachika muhtasari wa ripoti kwenye blogu ya Mtandao wa Afrika Magharibi wa Waandishi wa Habari Unaohusu Maji na Usafi wa Mazingira (WASH). Ripoti yenyewe ilishughulikia tathmini ya mahitaji ya baada ya maafa nchini Benin kufuatia mafuriko makubwa ya hivi karibuni. Maafa hayo yalisababisha vifo vya karibu watu hamsini na uharibifu uliokadiriwa kuwa FCFA bilioni 7.83 (karibu dola milioni 160) [fr]:

Siku hizi, wakati wowote ambapo mvua huanza kunyesha, ninaanza kuhisi hofu na wasiwasi,” Elizabeth Kpossou, mkaazi wa kijiji, anasema. Naye rafikiye na jiraniye, Alice Codjo, anahisi hivi. Hata hivyo, miaka michache iliyopita, mafuriko ya mara kwa mara yalikuwa matukio ya kawaida kwenye jamii hizo zenye amani. Na mbali na kuwa mapigo, mafuriko hayo yalipoisha, yaliacha udongo wenye rutuba. Nao wakaazi wa vijiji walichukua fursa kuutumia udongo huo. Sasa, siku hizo zimepita. “Kila kitu kikabadilika,” mkuu wa kijiji, Samuel Boton, anasema. “Sasa, mafuriko yanasababisha uharibifu mkubwa zaidi” [..] Kweli, kama ilivyo kwenye kijiji hiki cha Adjohoun chenye wakaazi 56,455, nchi nzima imekumbwa sana na maafa. Kote nchini, idadi ya vifo na kiasi cha uharibifu kilikuwa kikubwa mno. Kulikuwa na vifo 46 na zaidi ya nusu ya manispaa ziliathirika (manispaa 55 ziliathirika kati ya 77 zilizoko nchini Benin).

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.