- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Wazimbabwe Wamkejeli Tsvangirai Kwenye Mtandao wa Twita

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Zimbabwe, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho
Morgan Tsvangirai with Elizabeth Macheka cutting the wedding cake at at the Glamis Arena. Photo used with permission from nehandaradio.com

Morgan Tsvangirai akiwa na Elizabeth Macheka wakikata keki ya harusi kwenye viwanja vya Glamis. Picha imetumiwa kwa ruhusa ya nehandaradio.com

Wakati Waziri Mkuu wa zamani Morgan Tsvangirai akifukuzwa na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) kufuatia mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho, wa-Zimbabwe waliingia kwenye mtandao wa Twita na kutaniana kuhusiana na tukio hilo huku wengine wakiliita kuwa ni ‘janga la mwaka’.

Waasi ndani ya chama hicho wakiongozwa na Katibu Mkuu wa MDC Tendai Biti walimsimamisha Morgan Tsvangirai na vigogo wengine kwa tuhuma za kuzuia mabadiliko ya uongozi [1]na kushindwa kumng'oa rais Robert Mugabe. Tsvangirai anasema [2] kwamba yeye bado ni kiongozi wa chama hicho.

wa-Zimbabwe, wanaojiita “Twimbo”, walikuwa na kibarua cha siku nzima wakijaribu kupendekeza jina la kitabu cha kufikirika kumhusu Tsvangirai, na majina mengi yaliyopendekezwa yalikuwa ni utani mtupu.

@fingerray alianzisha majadiliano kwenye mtandao wa Twita yaliyowahamasisha Wazimbabwe kuwa wabunifu zaidi katika kujibu chemsha bongo hiyo:

Ninawapa chemsha bongo ya kupendekeza jina la kitabu cha Morgan baada ya balaa lililomkumba

Akitumia filamu ya “12 Years a Slave” na kipindi cha Tsvangirai akiwa kigogo wa MDC, @fingerray alitwiti:

Kiitwe miaka 15 ya utumwa

Akaandika tena:

Waliniambia ninafanana na Mandela

@ConorMWalsh akapendekeza:

Kiitwe Mfululizo wa Matukio ya Bahati Mbaya

@phirimarko akaandika:

Jamaa Ambaye Hangeweza Kuwa Mfalme

@jpmatengaalipendekeza kitabu cha kujifunza bila msaada wa mwalimu:

Namna ya kupoteza marafiki ndani ya siku 10

@__The_Duke alikuja na wazo geni:

Simulizi langu: Kutoka Kula Bata Mpaka Joto ya Jiwe

@George_Ruzv aliandika:

Mwisho wa Kila kitu

@DeltaNdou akaungana na wenzake:

“Kuwa taswira ya mapambano, na makalio ya kila masihara”

@RickyEMarima aliandika:

Usaliti Mkuu. Toleo la 2

@Cchabikwa alitumia jina na makao makuu ya MDC, yaitwayo Harvest House [Nyumba ya Mavuno:

Nyumba ya Miiba

@RickyEMarima alitamani jina la kitabu cha nguli wa riwaya “Things Fall Apart” lingekuwa bado halijatumika:

Nasikitika kuwa Jina la “Things Fall Apart” [Mambo yameharibika] limeshatumika.

@designartistic akaandika:

— Design Artistic (@designartistic) April 30, 2014 [33]

Kumwuua Ndege Aitwaye Morgan

@ChrisNqoe akapendekeza:

Bwana wa Dhoruba: Kurudi kwa Nikuv