- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ungana na Kampeni ya #FreeZone9Bloggers Twita Mei 14

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ethiopia, Naijeria, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Sheria, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

zonenine

Ungana na wanablogu wa Naijeria Blossom Nnodim (@blcompere [1]) na Nwachukwu Egbunike (@feathersproject [2]), pamoja na mhariri wa Global Voices Ndesanjo Macha (@ndesanjo [3]) kutoka Tanzania kwenye kampeni ya kutuma twiti barani Afrika kuwaunga mkono wanablogu na waandishi tisa waliokamatwa [4] mwishoni mwa mwezi Aprili na kwa sasa wanashikiliwa nchini Ethiopia.

Jumuiya ya Global Voices na mtandao wa marafiki na washirika wetu tunadai kuachiwa kwao, kwa kuwa walifanya kazi kwa bidii katika kupanua fursa ya uchambuzi wa kijamii na kisiasa nchini Ethiopia kupitia uandishi wa kiraia na ule wa kawaida. Tunaamini kukamatwa kwao ni kuvunja haki yao ya kimataifa ya uhuru wa kujieleza, pamoja na haki ya kutokukamatwa bila utaratibu. Unaweza kupitia habari hii na kampeni ya kuachiliwa kwao hapa [5].

Jumatano hii, kuanzia saa 8 mchana za Afrika Magharibi, tunapanga kutwiti kwa viongozi wa kijamii, serikali na wanadiplomasia, na vyombo vikuu vya habari (kwa kutumia anuani zao za twita) ili kufanya suala hili lisikike zaidi. Tunawahamasisha wanablogu na watumiaji wa mitandao ya kijamii barani Afrika kutuunga mkono –lakini kila mmoja anakaribishwa!

#FreeZone9Bloggers: Zoezi la kutuma twiti Kudai Kuachiliwa kwa Wanablogu wa Ethiopia Waliokamatwa 

Tarehe: Jumatano, Mei 14, 2014

Muda: Saa 8 – 11 jioni Kwa saa za Afrika Magharibi/ Saa 10 – 1 Jioni Kwa saa za Afrika Mashariki (bofya hapa [6] kujua itakuwa saa ngapi nchini kwako)

Alama Habari: #FreeZone9Bloggers

Waratibu: Blossom Nnodim (@blcompere [1]), Nwachukwu Egbunike (@feathersproject [2]), Ndesanjo Macha (@ndesanjo [3])

Ungana nasi Jumatano hii — twiti mpaka vidole vyako viume na dai kuachiliwa huru kwa wanablogu wa Zone 9!

Twiti unazoweza kutumia (bonyeza hapa kuchagua zaidi [7])