- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Njia 4 Unazoweza Kuzitumia Kujiunga na Kampeni ya #FreeZone9Bloggers

Mada za Habari: Ethiopia, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Utetezi
Zone 9 Tumblr Collage. [1]

Picha ya bango la Zone 9 Tumblr. Imetolewa wenye mtandao wa zoneniner.tumblr.com.

Befeqadu Hailu, Abel Wabela, Atnaf Berahane, Mahlet Fantahun, Zelalem Kibret, na Natnael Feleke (wote wakiwa n wanachama wa mkusanyiko wa wanablogu wa Zone 9) na waandishi wa habari Asmamaw Hailegeorgis, Tesfalem Waldyes pamoja na Edom Kassaye walikamatwa mnamo Aprili 25 na 26, 2014 jijini Addis Ababa. Tangu wakati huo, wamewekwa kizuizini kwenye mahabusu ya Maekelawi huku wakinyimwa haki ya kuonana na wanasheria. Vile vile hawaruhusiwi kuonana kabisa na familia zao.

Tangu mwaka 2012, wanablogu hao wa Zone 9 wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kuwezesha ushirikishwaji wa kiraia pamoja na uchambuzi wa kina kuhusu masuala ya kijamii na kisiasa nchini Ethiopia, wakifanya kazi sambamba na waandishi (ambao nao wamekamatwa) waliokuwa karibu nao ili kufikisha harakati hizo kwenye magazeti. Kukamatwa kwao kimsingi ni uvunjwaji wa haki za kimataifa zinazomlinda raia kujieleza, na haki yao ya kutokuteswa wakiwa chini ya ulinzi, kama Ibara ya 6 ya Makubaliano ya Afrika inavyotamka kuhusiana na masuala ya Haki za Binadamu na Makundi ya watu.

Jumuiya ya Global Voices na mtandao wetu wa marafiki na washirika tunadai kuachiliwa kwa ndugu zetu hao ambao idadi yao ni tisa.

Hapa ni namna nne ambazo wewe au shirika lako linaweza kuunga mkono kampeni hii:

1. Tuma barua: Mwandikie balozi wa Ethipia nchini kwako. Kama uko Afrika, andika kwa Ofisi ya Tume ya Afrika nchini mwako. Ni vizuri zaidi barua ifike kwa mkono!

2. Ongeza picha yako na ujumbe wa kuunga mkono kampeni hii kwenye mtandao wa  Free Zone 9 Tumblr [1]

3. Tia saini  Tamko la Jumuiya ya Global Voices [2] linalodai kuachiliwa huru kwa wanablogu hao

4. Sambaza ujumbe! Zungumza na rafiki zako, familia, na jamaa zako kuhusu kampeni hii — tuma makala na viungo vya habari, shirikiana nasi kwa kuandika barua kwa watunga sera au basi andaa, kama unaweza, mkutano wa kujadili masuala ya uhuru wa habari katika mji wako

 

Habari Maalumu za Global Voices kuhusu mashitaka ya wanablogu wa Zone 9

Mawakili Waiomba Tume ya Afrika, wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuingilia kati mashitaka ya wanablogu wa Zone 9 [3] Mei 3, 2014

TAMKO: Global Voices yatoa wito wa kuachiliwa kwa waandishi tisa nchini Ethiopia [2], Mei 2, 2014

Taarifa ya Watumiaji wa Mtandao: Ethiopia Yaminya Uhuru wa Maoni [4], Aprili 30, 2014

Wanachama sita wa Chama cha Kublogu Wakamatwa nchini Ethiopia [5], Aprili 25, 2014