- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mazungumzo ya GV: Maandamano ya ‘Alizeti’ Taiwan

Mada za Habari: Taiwan (ROC), Maandamano, Mahusiano ya Kimataifa, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia

Ungana nasi kwenye mazungumzo ya moja kwa moja kwa njia ya video kupitia mtandao wa Google Plus Mei 9, 2014 (Saa5:00 asubuhi UTC/GMT) [1]

Maua ya alizeti yamekuwa alama ya harakati za maandamano nchini Taiwani yanayoshinikiza mamlaka kamili ya nchi hiyo, katikati ya shinikizo la kisiasa la nchi hiyo kushirikiana zaidi na China.

Waandamanaji walivamia na kujaa kwenye bunge la nchi hiyo majuma kadhaa yaliyopita na walitumia mitandao ya kijamii kuwasiliana wao kwa wao kuhusu malengo yao na kuratibu shughuli kwa ubunifu wa hali ya juu.

Je, harakati hizo za kupigania demokrasia zina demokrasia ndani yake?

Kwenye mazungumzo ya GV leo tunazungumza na mwandishi wetu wa Taiwani I-Fan Lin [2] and Portnoy Zheng [3], mhariri mshiriki wa Global Voices Kichina [4] kuhusu namna maandamano hayo yalivyopokelewa nchini Taiwani.

Tazama pia:

Habari zetu maalumu za Global Voices kuhusu Maandamano ya Alzeti nchini Taiwani [5]