- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mazungumzo ya GV: Je, Utamaduni Ulisababisha Washindwe Kuokolewa Kwenye Ajali ya Kivuko?

Mada za Habari: Korea Kusini, Majanga, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vyombo na Uandishi wa Habari, GV Face

Ungana na mazungumzo haya moja kwa moja saa 8:30 alasiri kupitia teknolojia ya Google Plus [1].

Mitazamo potofu kuhusu Wakorea Kusini inaendelea kusambaa kwenye habari zinazotangazwa kuhusu kivuko kilichozama na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 200, wengi wao wakiwa ni vijana wa shule waliokuwa kwenye safari ya kimasomo. Je, wahanga hao walikuwa na utii uliopindukia kiasi cha kushindwa kuokolewa? Kwenye Mazungumzo ya GV leo tutazungumza na Mhariri wa timu yetu ya Kikorea Yoo Eun Lee [2] kuhusu mitazamo ya Wakorea juu ya taarifa zinazotangazwa na vyombo vya habari vya kimataifa kuhusiana na maana ya janga hilo kwao, na nani haswa wa kulaumiwa [3].

Soma pia: Wakorea Kusini Waituhumu Serikali kwa Kushindwa Kushughulikia Ajali ya Kivuko [3]