- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Maktaba na Utamaduni Huru

Mada za Habari: Amerika Kusini, Colombia, Elimu, Harakati za Mtandaoni, Uandishi wa Habari za Kiraia

Blogu kutoka Parque Biblioteca Tomás Carrasquilla – La Quintana, huko Medellin, Colombia, inaelezea [1] [es] msaada wake kwa utamaduni huru [2]. Baada ya kueleze namna ya kuleta utamaduni wa uhuru [3] [es], blogu hiyo inaelezea jinsi inavyoweza kufanya kazi inayofanana na maktaba:

Maktaba za umma zaweza kujifunza katika uhuru huu wa kubadilishana taratibu za ubunifu zilizofanywa ndani ya jamii wanazozihudumia, na hii inaweza kuwawezesha kwenye huduma za habari za mitaa, zilizoundwa kwa ushirikiano, zilizo shirikishwa, zilizoonekana na kupatikana kwa kila mtu ili maktaba nyingine, mashirika, vikundi vya utafiti na watu binafsi waweze kuwa na uwezo wa kuiga hayo, kuziboresha na kukabiliana nazo kwa mahitaji yao wenyewe na vifaa muhimu, hivyo kwa wakati wanaweza kutoa ule uzoefu wa awali na kutoa vyanzo mbalimbali kwa yale wamejifunza.

Makala yaliyopitiwa upya hapa ni sehemu ya kwanza [4] ya #LunesDeBlogsGV [Blogu ya Jumatatu kwenye GV] Mei 5, 2014, iliyowasilishwa [5] na María Juliana [6].