Beza Tesfaye anaelezea kwa nini kublogu ni tishio kwa serikali ya Ethiopia kufuatia kukamatwa kwa wanablogu tisa Ethiopia:
Ninapoandika haya, Kwa uwoga nakumbushwa kwamba nchini Ethiopia, kutoa maoni yako kunaweza kukufanya uakapewa tiketi ya daraja la kwanza gerezani.
Kutoka Aprili 25 hadi 26, 2014, wanablogu tisa wa Ethiopia na waandishi wa habari walikamatwa. Tulipokuwa tunasheherekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani siku ya Jumamosi, walikuwa kizuizini kwenye mahabusi mbaya zaidi jijini Addis Ababa. Ingawa madai hayajawasilishwa rasmi, kundi hilo limeshitakiwa kwa ” kufanya kazi na kutetea haki za binadamu wa kigeni” na “kutumia vyombo vya habari vya kijamii kufanya nchi isitulie”. Kama watashitakiwa chini ya sheria ya Ethiopia ya kukabiliana na ugaidi, wanaweza kukabiliwa na adhabu ya kifo.
Kukamatwa kwao ni sehemu ya mwenendo wa kuhofia nchini Ethiopia, ambayo mara nyingi imewekwa katika nafasi ya kama moja ya maeneo yenye kandamizi kwa uhuru wa vyombo vya habari katika miaka ya hivi karibuni.