- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Ethiopia: #FreeZone9Bloggers Yavuma Kwenye Mtandao wa Tumblr

Mada za Habari: Ethiopia, Haki za Binadamu, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza

tumblr_n575s45oAT1tacd1co1_1280 Global Voices Advocacy ilianzisha mtandao wa Tumblr [1] mapema mwezi Mei kutafuta uungwaji mkono kwa wanablogu tisa na waandishi wa habari – ambao wanne kati yao ni wanachama wa Global Voices – ambao kwa sasa wako kizuizini nchini Ethiopia [2] shauri ya kazi zao. Washirika kutoka duniani kote waliwasilisha picha, ujumbe wa mshikamano, video na michoro kuonyesha kuunga mkono shinikizo hilo la kuachiliwa huru kwa wanablogu hao. Mei 19 #FreeZone9Bloggers Tumblr [1] ilianza kuvuma katika tovuti ya vyombo vya habari vya kijamii. Unaweza kuwasilisha picha [3] kwa Tumblr au jifunze njia nyingine [4] unazoweza kuzitumia kusaidia kampeni hiyo ya utetezi.