- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Colombia: Hatua za Kudhibiti Mashambulizi ya Kemikali

Mada za Habari: Amerika Kusini, Colombia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Ili kuepusha mashambulizi ya kemikali [1] yanayowalenga hasa wanawake katika maeneo mbalimbali ya nchi, serikali ya Colombia itaanza kudhibiti [2] [es] mauzo ya rejareja ya kemikali ya ‘chokaa’ na vitu vya kemikali kama salfa, haidrokloriki, mariati, chokaa, naitriki na sodiamu haidroksaidi, katika hali ya kimiminika na vipande

RCN Radio [3] ilitoa taarifa kwenye mtandao wa Twita:

Serikali inaandaa amri ya kudhibiti uuzaji wa kudhibitiwa wa kemikali.