- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Caribbean Yajiunga na Kampeni ya #BringBackOurGirls

Mada za Habari: Nchi za Caribiani, Naijeria, Trinidad na Tobago, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Maandamano, Sheria, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Ubaguzi wa Rangi, Vijana, Vyombo na Uandishi wa Habari, Wanawake na Jinsia

Kama watoto wetu wangetoweka tungelipenda dunia yote kusimama na kuja kutusaidia kuwatafuta wao. Sisi … tunauliza kwamba … kwa nini mara nyingi miili ya wanawake huwa uwanja wa vita ambapo vita hupiganiwa. Hili si tatizo ambalo linahusisha mji mdogo nchini Nigeria, ni tatizo la wasichana wote kila mahali.

Tillah Willah [1] alimwandikia barua Goodluck Jonathan, kutoa wito wa kulichukulia suala la “kupotea kwa wasichana 234 wa shule ya Chibok, Borno … kwa umakini na uharaka zaidi.”