- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Waethiopia Waadhimisha Siku ya Wajinga kwa Kuikejeli Televisheni ya Taifa

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Ethiopia, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Vichekesho, Vyombo na Uandishi wa Habari

Waethiopia walisherehekea Siku ya Wajinga [1] kwenye mtandao wa Twita kwa kusambaza vichwa vya habari za uongo zilizokuwa zikiiga "uongo" wa kituo cha televisheni cha taifa cha nchi hiyo (ETv), ambacho ndicho kituo pekee cha televisheni cha taifa katika nchi hiyo ya Afrika. Kwa kutumia alama habari #ETvDay [2], watumiaji wa mtandao walikituhumu kituo cha ETv kwa "kudanganya kwa siku 365 za mwaka".

Yote hayo yalianzia kwenye picha hii hapa chiniw:

ETv imefanikiwa kuingia kwenye orodha ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa

Jomanex [5] alibainisha kwa lugha ya ki-Amariki:

Soli [10] alitania kuhusu uchaguzi mkuu ujao wa 2015:

Uchaguzi ujao utakuwa huru, haki na wa kidemokrasia

Uchaguzi wa nchi hiyo wa 2005 ulivurugwa na kuishia na maandamano mtaani [14], ambapo watu 193 waliuawa na zaidi ya wengine 30,000 kukamatwa na vyombo vya usalama. Mwaka 2010, uchaguzi [15] ulikipa ushindi wa kishindo chama kinachotawala nchi hiyo cha [PRDF] People's Revolutionary Democratic Front, kilichopata asilimia 99.6 ya viti bungeni. Upinzani uliyakataa matokeo hayo na waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo haukukidhi wiwango vya kimataifa.

Ni wazi, Ethiopia itafanikiwa kufikia moja wapo ya Malengo ya Kimaendeleo ya Milenia [16] - jumla ya malengo ya kimaendeleo yalikubalika kwenye mkutano wa Milenia wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000 - mkutano ulikuwa wa kihistoria:

Vyanzo vinasema kuwa Ethiopia itaweza kutoa huduma maji safi ya kunywa kabla ya tarehe ya mwisho ya kufikiwa kwa malengo ya Milenia.

Wakazi wa mtaa wa Gulelle ambao hawakuweza kupata maji kwa siku 20 zilizopita wamesema hawajapata mafunzo ya namna ya kuishi bila maji.

Kuhusu kura ya maoni ya Crimea, ambapo mkoa huo wa Ukraine ulipiga kura ya kishindo ya kujitenga na Urusi:

Baadhi ya wakazi wa Adama [jiji lililoko katikati ya nchi hiyoa] wamesema kujitenga kwa Crimea na kujiunga Urusi hakutaathiri Ukuaji na mipango ya Mabadiliko ya Ethiopia.

Mahlet [22] aligawanya habari katika makundi mawili:

BefeQadu akaongeza [24]:

Kuna aina mbili za watu duniani: wale wanaoitazama ETv kila siku na wale waliokolewa na Mungu kuepushwa kuitazama

Kw akutumia kauli mbiu ya zamani ya Tume ya Utalii ya Ethiopia, "Miezi 13 ya mwanga wa jua", Saleh [26] alisema:

Miezi 13 ya mwangaza wa jua; miezi 13 ya uongo wa serikali kwenye kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali = Siku ya wajinga

Hivi siku ngapi za mwaka zinamilikiwa na ETv?:

Oromo Network's [32] wished:

Furahia twiti nyinginezo nyingi za #ETvDay  hapa [35].