Waethiopia walisherehekea Siku ya Wajinga kwenye mtandao wa Twita kwa kusambaza vichwa vya habari za uongo zilizokuwa zikiiga "uongo" wa kituo cha televisheni cha taifa cha nchi hiyo (ETv), ambacho ndicho kituo pekee cha televisheni cha taifa katika nchi hiyo ya Afrika. Kwa kutumia alama habari #ETvDay, watumiaji wa mtandao walikituhumu kituo cha ETv kwa "kudanganya kwa siku 365 za mwaka".
Yote hayo yalianzia kwenye picha hii hapa chiniw:
ETv made it to the UN international days list. #ETvDay in #EtvStyle. By @jomanex pic.twitter.com/8hMK76uWS8
— BefeQadu Z Hailu™ (@befeqe) March 31, 2014
ETv imefanikiwa kuingia kwenye orodha ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa
Jomanex alibainisha kwa lugha ya ki-Amariki:
አፕሪል ዘፉል የፈረንጅ ነው ኢቲቪ ግን <<የኛ>> ነው፡፡ ከስተማይዜሽን #EtvDay
— Jomanex Kassaye (@jomanex) April 1, 2014
Soli alitania kuhusu uchaguzi mkuu ujao wa 2015:
The coming 2015 national election is fair, free and democratic. #ETVday. #Ethiopia
— Soli ሶሊ (@Soli_GM) April 1, 2014
Uchaguzi ujao utakuwa huru, haki na wa kidemokrasia
Uchaguzi wa nchi hiyo wa 2005 ulivurugwa na kuishia na maandamano mtaani , ambapo watu 193 waliuawa na zaidi ya wengine 30,000 kukamatwa na vyombo vya usalama. Mwaka 2010, uchaguzi ulikipa ushindi wa kishindo chama kinachotawala nchi hiyo cha [PRDF] People's Revolutionary Democratic Front, kilichopata asilimia 99.6 ya viti bungeni. Upinzani uliyakataa matokeo hayo na waangalizi wa kimataifa walisema uchaguzi huo haukukidhi wiwango vya kimataifa.
Ni wazi, Ethiopia itafanikiwa kufikia moja wapo ya Malengo ya Kimaendeleo ya Milenia - jumla ya malengo ya kimaendeleo yalikubalika kwenye mkutano wa Milenia wa Umoja wa Mataifa mwaka 2000 - mkutano ulikuwa wa kihistoria:
"ኢትዮጵያ የንፁህ መጠጥ ውሃ አቅርቦትን ከምዕተ አመቱ ግብ ቀድማ እንደምታሳካ አንዳንድ ውስጥ አዋቂ ምንጮች ገለፁ" #ETvDay (Picha Arsi/Ethiopia - 2013) pic.twitter.com/GZ7iF9JvFx
— Zelalem Kibret (@zelalemkibret) April 1, 2014
Vyanzo vinasema kuwa Ethiopia itaweza kutoa huduma maji safi ya kunywa kabla ya tarehe ya mwisho ya kufikiwa kwa malengo ya Milenia.
#Etvday በጉለሌ ክፍለ ከተማ የሚገኙ ነዋሪዎች ከ20 ቀናት በላይ የመጠጥ ውሃ ማግኘት ባይችሉም፥ ልማታዊው መንግስታችን ያለ መጠጥ ውሃ እንዴት መኖር እንደሚቻል አስቀድሞ ስልጠና ስለሰጠን ተጎጂ አልሆንም ሲሉ ገለፁ።
— Tewodros Belay (@tewodros_belay) April 1, 2014
Wakazi wa mtaa wa Gulelle ambao hawakuweza kupata maji kwa siku 20 zilizopita wamesema hawajapata mafunzo ya namna ya kuishi bila maji.
Kuhusu kura ya maoni ya Crimea, ambapo mkoa huo wa Ukraine ulipiga kura ya kishindo ya kujitenga na Urusi:
ሩሲያ ክሬሚያን የራሰዋ ግዛት ማድረግ ፤ ኢትዮጵያን ከእድገትና ትራንስፎርሜሽን እንደማያደናቅፋት አንዳንድ የአዳማ ነዎሪዎች ተናገሩ #ETvDay
— Yassin Nuru (@yassinahmed1) April 1, 2014
Baadhi ya wakazi wa Adama [jiji lililoko katikati ya nchi hiyoa] wamesema kujitenga kwa Crimea na kujiunga Urusi hakutaathiri Ukuaji na mipango ya Mabadiliko ya Ethiopia.
Mahlet aligawanya habari katika makundi mawili:
There is news and there is ETV news. #ETvDay
— Mahlet (@Mahlet_S) April 1, 2014
Kuna habari na kuna habari za ETv [televisheni ya taifa hilo]
BefeQadu akaongeza:
የዓለም ሕዝብ በሁለት ይከፈላል፤ ኢቴቪ በየቀኑ የሚያይ እና እግዜር ያተረፈው። #ETvDay
— BefeQadu Z Hailu™ (@befeqe) April 1, 2014
Kuna aina mbili za watu duniani: wale wanaoitazama ETv kila siku na wale waliokolewa na Mungu kuepushwa kuitazama
Kw akutumia kauli mbiu ya zamani ya Tume ya Utalii ya Ethiopia, "Miezi 13 ya mwanga wa jua", Saleh alisema:
13 months of sunshine & 13 months of government lies on a state-owned TV station. #ETvDay = April the fool @BBCAfrica @AJStream
— saleh (@2zworld) April 1, 2014
Miezi 13 ya mwangaza wa jua; miezi 13 ya uongo wa serikali kwenye kituo cha televisheni kinachomilikiwa na serikali = Siku ya wajinga
Hivi siku ngapi za mwaka zinamilikiwa na ETv?:
In response to allegations by activists that today is #ETVday, ETV announced today is the only day of the year that it does not own. #April1
— Bon Bon (@BonayaBonso) April 1, 2014
Katika kujibu shutuma za wanaharakati hao siku hiyo, ETV ilitangaza kuwa hii [siku ya wajinga] ndio siku pekee ambayo haiimiliki.
Oromo Network's wished:
I expect mass resignation by ETV journalists today. #ETvDay #13monthsofEtvlies
— Oromo Network (@Oromo_NT) April 1, 2014
Ninategemea waandishi wengi wa ETv wataacha kazi kwa mpigo
Furahia twiti nyinginezo nyingi za #ETvDay hapa.
2 maoni