- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

VIDEO: Wimbo wa ‘Furaha’ wa Pharrell Williams na Taswira Halisi ya El Salvador

Mada za Habari: Amerika Kusini, El Salvado, Habari Njema, Muziki, Uandishi wa Habari za Kiraia

Wananchi wa Salvador wametengeneza toleo lao la wimbo “Happy [1]” [furaha] ulioimbwa na Pharrell Williams. Mwanablogu Mildred Largaespada anaisifu video hiyo kwenye ukurasa wake wa Facebook [2] [es]:

ni nzuri. Na ndiyo, kama ilivyo kwenye maisha halisi, video hii ni halisi: wakati mwingi wa siku, wanawake na wanaume wa El Salvador wanaoneka kuwa na furaha na kwa hakika hawana msongo wa habari mbaya zinazotangazwa kwenye taarifa za vyombo vya habari na kuzinya zionekane ni halisi kuliko ukweli unaonekana kwenye video hii.

Video [3] ilipandishwa mtandaoni na mtumiaji wa mtandao wa YouTube El Salvador Happy [4]: