- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Tetemeko la Ardhi la Ukubwa wa 6.2 Latokea Nchini Nicaragua

Mada za Habari: Amerika Kusini, Nicaragua, Majanga, Uandishi wa Habari za Kiraia

Tetemeko la ardhi lenye nguvu ukubwa wa 6.1 lilitokea [1] Nicaragua mnamo Alhamisi Aprili 10, 2014. Kulikuwa na taarifa [2] [es] za watu kujeruhiwa na kuanguka kwa nyumba shauri ya mtikisiko mkubwa.

Kitovu kilikuwa kilomita 20 Kaskazini ya mji mkuu Managua, karibu na volkano ya Apoyeque, wa kina cha kilomita 10. Katika mtandao wa Twita, watumiaji waliripoti tetemeko dogo na kusimamishwa kwa shughuli za shule:

Tetemeko la tano baada ya tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.2 nchini Nicaragua: MANAGUA, Nicaragua.- Angalau…

Shughuli za shule kusimamishwa katika Managua [6] na León kutokana na tetemeko la ardhi..