- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Serikali Mpya ya Waziri Mkuu Roger Kolo Yatangazwa Nchini Madagaska

Mada za Habari: Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara, Madagaska, Habari Njema, Habari za Hivi Punde, Siasa, Uandishi wa Habari za Kiraia, Utawala

Mtandao wa Tananews nchini Madagascar umechapisha orodha kamili ya mawaziri 31 wa serikali mpya ya Madagaska [1] [fr]. Mitsangana Madagascar anasema kwamba orodha hiyo ina wanawake 6 na kuwa mawaziri 7 walikuwa kwenye baraza [2][fr] la serikali iliyopita ya mpito. Waziri mkuu wa zamani Beriziky aliitakia serikali kila la heri kwenye mtandao wa Twita:

Namuwasilisha Roger Kolo (@kolo_roger) kama waziri mkuu mpya. Shukrani nyingi kwa Malagasies wote #Madagascar