Rais Mugabe Anadhani Naijeria Inanuka Ufisadi Kuliko Zimbabwe

President Robert Mugabe. Public Domain photo belonging to U.S. Air Force.

Rais Robert Mugabe. Picha ya matumizi ya umma na ni mali ya Jeshi la Anga la Marekani.

Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameikasirisha Naijeria kwa matamshi aliyoyatoa Machi 15, 2014 wakati wa sherehe ya kuzaliwa kwake kuwa Naijeria na raia wake ni mafisadi.

Mugabe aliuliza, “Hivi tumekuwa kama Naijeria nchi ambayo ni lazima upapase mfuko ili kupewa huduma yoyote? Unajua, tumekuwa tukienda Naijeria na kila wakati tukienda kule ilitubidi kubeba pesa za ziada mifukoni mwetu ili kutoa rushwa kwa kila tulichotaka kukifanya. Unapanda ndege nchini Naijeria na unakaa kwenye siti na wafanyakazi wa ndege wanabaki kujibaraguza na ndege haiondoki utadhani wanasubiri uwalipe ili ndege ipae.”

Serikali ya Naijeria imemwandikia balizi wa Zimbabwe wiki iliyopita kupata ufafanuzi wa matamshi hayo ya Mugabe. Hata hivyo, Umoja wa Kupambana na Watawala Mafisadi (CACOL) nchini Naijeria umeitaka serikali ya shirikisho kufanyia kazi ujumbe huo na sio aliyeutoa ujumbe huo. 

Kipimo cha Ufisadi kwa mwaka 2013 cha taasisi ya Transparency kinaonyesha kiwango cha ufisadi unaoonekana kiko juu zaidi nchini Zimbabwe kuliko ilivyo Naijeria.

Matamshi ya Mugabe yamesababisha joto la maoni mbalimbali kwenye mtandao wa Twita. Baadhi ya watumiaji wa mtandao walidai alichosema kina ukweli:

Alisema kweli, kweli tupu :) Naijeria kutuhumiwa ndiyo habari sio Mugabe

Mugabe amewatuhumu Wazimbabwe kubadilika kuwa kama Naijeria linapokuja suala la ufisadi. Ni simulizi la jiko kuliita sufuria jeusi

Robert Mugabe yuko sawa kabisa kwa maneno yake kuhusu Naijeria

Kile Mugabe alichosema kuhusu Naijeria ni ukweli ila aliyasema hayo kwa watu wasio sahihi

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, kwa nini Robert Mugabe anaipaka matope Naijeria. Ni kweli kuwa Wanaijeria ni wananuka rushwa?

Mugabe anasema “Wanaijeria wote ni wala rushwa” wakati benki ya dunia imeonesha kuwa “Naijeria ni nchi masikini zaidi barani Afrika” Umasikini = ufisadi

Ufisadi ni tatizo kubwa Naijeria. Watawala wetu ni mafisadi kupindukia. Simlaumu Mugabe kwa makonde yake dhidi ya nchi yetu

Naijeria imemtaka balozi wa Zimbabwe kutoa maelezo kuhusiana na matamshi hayo ya Mugabe. Mimi ni Mnajieria lakini sioni kosa lolote kusema ukweli

La! Kama Mugabe anaweza kufungua mdomo wake kuuita Naijeria kuwa inanuka rushwa….basi ni wazi tunalo tatizo kubwa…tena kubwa sana!

@figure007 alidhani kuwa Mugabe alisema ukweli, ingawa hana uhalali wa kimaadili:

Nimesoma kile alichokisema Mugabe kuhusu Naijeria, ingawa alisema ukweli, lakini hana uhalali wa kimaadili kusema hayo kama Rais aliye madarakani

Wengine hawakukubaliana na maoni yake kuhusu ufisadi nchini Naijeria:

Ujasiri wa hali ya juu. Mugabe anaiita Naijeria inanuka rushwa? Da! Ibilisi tunayemjua ni mdogo mno kukabiliana na kizee hiki cha miaka 90!

Nini maana ya kukitoa kibanzi kwenye jicho lako mwenyewe? Matamshi ya Robert Mugabe yanaichokoza Naijeria

Mugabe anathubutu kusema Serikali ya Naijeria inanuka ufisadi? Serikali ya Naijeria ina haki ya kuona imedhalilishwa

Chungu kuliita jiko kuwa ni jeusi. Zote ni nchi zinazonuka ufisadi. Matamshi ya Mugabe yanaitukana Naijeria tu

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.