Mwanablogu wa Iran Aliyefungwa Aandika Barua Kuelezea Anavyoteswa

Jailed since

Mwanablogu wa Iran Siamak Mehr aliwekwa kizuizini mwaka 2010 na kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka minne jela

Mohammad Reza Pourshajari, mwanablogu aliyefungwa hela anayefahamika kwa jina lake la kalamu Siamak Mehr, aliandika barua ya wazi kutoka jela ambapo alizungumzia vitendo vya utesaji na hali ngumu anayokabiliana nayo gerezani. Barua hiyo, yenye tarehe Machi 6, 2014 ilichapishwa kwenye tovuti nyingi mwisho wa mwezi Machi.

Mwanablogu huyo mwenye miaka 52 anatumikia kifungo chake cha miaka minne kwenye gereza la Ghezel Hesar mjini Karaj, ulioko kaskazini magharibi mwa Tehran. Alikamatwa Sepatemba 12, 2010 kwa mashtaka ya kumkashfu Mtume Muhammad na kumkufuru Mungu kwenye makala alizokuwa anaziweka kwenye blogu yake.

Kwenye barua hiyo, Pourshajari aliandika:

… mara tu nilipowekwa chini ya ulinzi nyumbani kwangu na vyombo vya usalama, niliteswa, nilipigwa na kutishiwa kifo…mimi ni mhanga wa unyanyasaji wa utawala huu wa Kiislamu. Nilihukumiwa miaka minne gerezani kwa kuandika kuhusu haki na ukiukwaji wa haki za raia [wa Iran]…ninaandika barua hii nikiwa kwenye chumba kidogo chenye eneo la mita 21 mraba nikiwa na wafungwa wengine 40 ambao wengi ni wahalifu, wabakaji, watumiaji wa mabawa ya kulevya…Nchi hii ya Kiislamu inakiuka haki za msingi za kiraia na kuwanyang'anya watu uhuru.

Mwisho wa barua hiyo, anawakaribisha jumuiya na serikali za Kimataifa zinazojali haki za binadamu kuwasaidia wananchi wa Iran kupata haki zao na uhuru.

Binti wa mwanablogu huyo, Mitra Pourshajari, aliandika barua mwezi Februari 2014, akieleza/a> kuwa maisha ya baba yake yako hatarini. Alisema:

Serikali inakataa kumsafirisha Bw. Pourshajari kwenda kupata huduma za matibabu na wanamnyima huduma hiyo, ili apoteze maisha. Kwa [mamlaka za gereza], ushauri wa daktari hauna maana; wanapuuza ushauri….Raia wa Iran wanalazimika kuheshimu na kufanya lolote ili kupendezesha mfumo wa serikali.

Ukurasa wa Facebook umeanzishwa ili kumwunga mkono mwanablogu huyo aliyefungwa, ukiwa na nakala ya barua zake na habari mpya zinazohusiana na hali yake.

Hapa chini ni video, iliyowekwa mtandaoni Desemba 2011, ikimwonyesha Siamak Mehr akiwa amefungwa minyororo, akielekea mahakamani.

1 maoni

  • Kiungo cha makala haya kutokea kwenye tovuti nyingine: Mwanablogu wa Iran Aliyefungwa Aandika Barua Kuelezea Anavyoteswa | TravelSquare

    […] Mwanablogu wa Iran Aliyefungwa Aandika Barua Kuelezea Anavyoteswa Mwanablogu wa Iran Siamak Mehr aliwekwa kizuizini mwaka 2010 na kwa sasa anatumikia kifungo cha miaka minne jela Mohammad Reza Pourshajari, mwanablogu aliyefungwa hela anayefahamika kwa jina lake la kalamu Siamak Mehr, aliandika barua ya wazi kutoka jela ambapo alizungumzia vitendo vya utesaji na hali ngumu anayokabiliana nayo gerezani. Barua hiyo, yenye tarehe Machi 6, 2014 ilichapishwa kwenye tovuti nyingi mwisho wa mwezi Machi. Mwanablogu huyo mwenye miaka 52 anatumikia kifungo chake cha miaka minne kwenye gereza la Ghezel Hesar mjini Karaj, ulioko kaskazini magharibi mwa Tehran. Alikamatwa Sepatemba 12, 2010 kwa mashtaka ya kumkashfu Mtume Muhammad na kumkufuru Mungu kwenye makala alizokuwa anaziweka kwenye blogu yake. Kwenye barua hiyo, Pourshajari aliandika: … mara tu nilipowekwa chini ya ulinzi nyumbani kwangu na vyombo vya usalama, niliteswa, nilipigwa na kutishiwa kifo…mimi ni mhanga wa unyanyasaji wa utawala huu wa Kiislamu. Nilihukumiwa miaka minne gerezani kwa kuandika kuhusu haki na ukiukwaji wa haki za raia [wa Iran]…ninaandika barua hii nikiwa kwenye chumba kidogo chenye eneo la mita 21 mraba nikiwa na wafungwa wengine 40 ambao wengi ni wahalifu, wabakaji, watumiaji wa mabawa ya kulevya…Nchi hii ya Kiislamu inakiuka haki za msingi za kiraia na kuwanyang'anya watu uhuru. Mwisho wa baru… Kusoma makala kamili  »  http://sw.globalvoicesonline.org/2014/04/mwanablogu-wa-iran-aliyefungwa-aandika-barua-kuelezea-anavyoteswa/ […]

jiunge na Mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.