Mkutano wa Global Voices Jijini Lagos, Naijeria

gvmeetuplogo1Mikutano ya Global Voices imeanza kwa mwaka 2014. Kufuatia mafanikio ya mikutano kwenye majiji sita duniani kote mwaka 2013, wanafamilia wa Global Voices wanafanya juhudi za kuandaa fursa kwa wasomaji wetu na wengine wote wanapenda kujifunza zaidi kuhusu kazi zetu kuhusika na shughuli zetu. Tunayo furaha kubwa kutangaza mkutano wetu mdogo unaopagwa kufanyika Alhamisi ya Aprili 17 jijini Lagos, Naijeria.

Mwenyeji wa mkutano huo atakuwa ni mwanafamilia ya Global Voices Nwachukwu Egbunike (@feathersproject) akishirikiana na Shule Kuu ya Mawasiliano ya Umma ya Chuo Kikuu cha Pan-Atlantic katika kisiwa cha Victoria, Lagos kuanzia saa 3:00 asubuhi. Usajili unahitajika (tazama hapa chini kwa taaarifa zaidi).

Mkutano huo utakuwa ni fursa kwa wanafunzai, wanablogu, na wengine wanaofanya kazi katika tasnia ya uandishi wa kiraia kushirikiana uzoefu wao na kujifunza zaidi kazi za wengine. kwa nyongeza, tukio litakuwa na malengo yafuatayo:

  • Kutoa picha ya kazi ambazo tunazifanya kwenye Global Voices, ikiwa ni pamoja na miradi maalumu ya Rising Voices, Advox, na Lingua
  • Kushirikiana njia ambazo jamii kwa upana wake inaweza kuhusika na Global Voices
  • Kutengeneza mtandao ili washiriki waweza kushirikiana taarifa kuhusu miradi yao ya kidijitali au hata mawazo waliyonayo kwa miradi ijayo
  • Majadiliano kuhusu namna ya kuthibitisha habari kwenye mitandao ya kijamii

Kama ungependa kushiriki, tafadhali jaza fomu ifauatayo ya usajili. Utapokea uthibitisho wa barua pepe kuhusu ushiriki wako. Tukio hili ni bure, ingawa nafasi ni chache. Unaweza kutuma barua pepe kwa: rising [at] globalvoicesonline.org kwa ajili ya taarifa zaidi. Tafadhali fuatilia alama habari ya #GVMeetup kwa ajili ya kujua zaidi kuhusu mikutano hii na mingineyo ijayo duniani kote.

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.