- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mazungumzo ya GV: “Mtandao wa Twita” wa Siri wa Kimarekani Nchini Cuba

Mada za Habari: Cuba, Marekani, Pakistan, Habari za Hivi Punde, Haki za Binadamu, Harakati za Mtandaoni, Mahusiano ya Kimataifa, Teknolojia, Uandishi wa Habari za Kiraia, Uhuru wa Kujieleza, Utawala, GV Face

Mpango wa siri wa Marekani wa kubadili utawala nchini Cuba wenye huduma ya ujumbe inayofanana na Twita iitwayo ZunZuneo [1] sasa unaangaliwa kwa mashaka baada ya kuwepo kwa taarifa kuwa maelfu ya wa-Cuba walidanganyika kujisajili kupata huduma hizo.

Je, kutakuwa na madhara kwa wanaharakati wa kidijitali duniani kote? Wengine wana mashaka gatua hiyo inaweza kusababisha hali ya kutokuaminiana na kufuatiliwa kwa mtandao wa intaneti na mitandao ya kijamii katika nchi zao.

Majadiliano ya kina na: Sana Saleem [2], Ivan Sigal [3] na Solana Larsen [4].