- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Mashabiki Jijini Skopje Wakusanyika Kubadilishana ‘Stika’ za Soka

Mada za Habari: Ulaya Mashariki na Kati, Macedonia, Habari Njema, Mawazo, Michezo, Uandishi wa Habari za Kiraia

Mamia ya watu walikusanyika mchana wa Jumapili kwenye eneo la wazi jijini Skopje kubadilishana ‘stika’ za mkusanyiko rasmi wa picha za Kombe la Dunia la FIFA tarehe 28 Aprili, 2014.

Sticker exchange in Skopje, Macedonia on April 27, 2014. [1]

Watu wa rika zote wakibadilishana ‘stika’ kwenye bustani ya wazi jijini Skopje. Picha: F.S. (CC-BY)

Nchini Macedonia, kama ilivyo kwa nchi nyinginezo za Yugoslavia ya zamani, utamaduni wa kukusanya ‘stika’ una historia ndefu, inaanzia miaka ya 1970 na albamu za ‘stika’ sasa zinauzwa. Watu wazima hushiriki kubadilishana ‘bidhaa’ hiyo sambamba na watoto na matoleo yaliyo maarufu ni pamoja Panini [2] zinazotoka Italia na Kraš [3] (Kundi la wanyama) zinazotoka Kroashia. Mwaka 2006, mtengeneza program za kompyuta aitwaye Goran Slakeski alianzisha tovuti za slikicki.com [mk [4], en [5], si [6]] ambazo zimekuwa kitovu cha jamii ya watu wanaopenda kubadilishana ‘stika’, akipanua wigo mara chache kwenda kwenye matukio halisi mtaani kama hili lililofanyika.