Maelfu Wamiminika Kumwona Yesu ‘Aliyetokea’ Nchini Cameroon

Wakati wa Jiji la Yaounde, mji mkuu wa Cameroon, siku ya Jumatano ya Aprili 16, 2014 waliamshwa na habari kuwa sura ya Yesu Kristo imetokea katika nyumba moja iliyoko mtaa wa Odza. Habari hizi ziliibua hisia za  maelfu ya watu [fr] waliomiminika kuelekea mitaa hiyo kujionea [fr] muujiza wa Pasaka kwa macho yao wenyewe.

Siku chache baadae, Mhashamu Askofu Mkuu wa Douala Samuel Kleda, alitupilia mbali [fr] madai ya muujiza huo akiuita maigizo, lakini hata hivyo, kauli hiyo haikuwazuia watu hao kuendelea kumiminika kwenda kwenye nyumba hiyo ya Amougui Minkan. Baadhi yao waliamua kuruka fensi iliyokuwa imezunguka nyumba hiyo kukwepa mistari mirefu ilikuwa ikisubiri kuingia nyumbani humo.

Habari za kuonekana “kwa Yesu” ghafla zikawa habari kubwa kwenye mtandao wa Twita nchini cameroon ambapo watumiaji walitwiti madai hayo katika hali ya kutokuamini na utani.

Mwanablogu@ngimbis alihoji kile hasa walichokuwa wakikiona watu kwenye ukuta:

Jamani! Utahitaji vifaa maalumu kukusaidia kumwona, eti?

Wengi walichukulia tukio hilo kuwa ni masihara tu kwamba Yesu aamue kutokea Cameroon badala ya maeneo mengine:

Kwamba Yesu amerudi? Ha ha! Hata kama Yesu atarudi tena hawezi kuingilia kupitia cameroon…haiwezekani!!

Ukweli kwamba ‘ufunuo’ huo ulitokea Odza, mtaa ulio karibu na Nsimalen, mtaa ambao Mariamu, mama wa Yesu aliwahi kuripotiwa kutokea, mwaka 1986 ulimaanisha jambo kwa wengi:

Ni dhahiri, Yesu na mama yake wameamua kuhamia kwenye mitaa inayofuatana. Cameroon imebarikiwa

@ntrjack hakujizuia kurudia mdahalo wa enzi na enzi kuhusu rangi ya Yesu:

Kwa hiyo Yesu ni mzungu kila anapotokea. Basi mjadala umehitimishwa rasmi

Na @lesikanel alitania:

Bado ninamsubiri mtu aweke posti yenye picha yake akiwa na Yesu pale Odza

Kwa wengine, kutokea huko kulikuwa fursa ya uchambuzi wa masuala ya kijamii na kisiasa. Kwa @TjatBass, Yesu kutokea Younde haikuwa na maana yoyote:

Yesu kweli anaipenda Cameroon! Lakini bado kuna kisichoeleweka, mbona kuna vitendo vingi vya kuminywa kwa haki na wengi bado wanakufa?

@ngimbis Kwa upande mwingine aliwakumbusha wananchi wa Cameroon kuwa rais Paul Biya bado hajaonekana wala kusikika tangu ahudhurie Mkutano Mkuu wa Umoja wa Ulaya jijini Brussels mnamo  Aprili 2-3, 2014:

Kama akipatikana, Yesu wa Odza itabidi atumikie nchi yetu kama rais wa muda kwa sababu rais wetu haonekani tangu Mkutano wa Umoja wa Ulaya.

Biashara imeshamiri kwenye mitaa ya Odza tangu Yesu aonekane huko. Wakionekana kutokutaka kuachwa nyuma, wamiliki wa nyumba ambapo Yesu anasemekana kuonekana, hivi sasa wanadai michango:

Yesu mwana wa Mungu ameonekana Yaounde, Cameroon wakati wa wiki takatifu ya Pasaka. Ameonekana nyumbani. Hivi sasa kuna kiingilio ukitaka kumwona.

Wiki moja baada ya tukio hilo la Yesu kuonekna Odza liripotiwe, wengi bado wanamiminika kwenda kuhiji eneo hilo [fr] la Odza wakatimjadala kuhusu ukweli wa tukio hilo ndio kwanza umepamba moto. Hata hivyo, mtazamo unaotawala mjadala huo umetolewa na @Difredsimpson anayesema:

Yesu Kutokea Yaounde? Ha ha ha haa! Ni upuuzi wa mwezi huu

Anza mazungumzo

Mwandishi, tafadhali jiandikishe »

Miongozo

  • Tafadhali wape heshima watumiaji wengine. Maoni yenye lugha ya chuki, matusi na mashambulizi binafsi hayataruhusiwa.