- Global Voices in Swahili - https://sw.globalvoices.org -

Kurekebisha Historia: Sauti ya Wahanga Waliolazimishwa Kuwa ‘Wagumba’ Nchini Peru

Mada za Habari: Amerika Kusini, Peru, Afya, Uandishi wa Habari za Kiraia, Wanawake na Jinsia

Likiwa na lengo la kukusanya saini 3,000, shirika la MujeresMundi [1] limeanzisha madai ya mtandaoni kwenye jukwaa la Change.org [2] likiitaka serikali ya Peru kujenga upya kumbukumbu ya kihistoria kwa sauti ya wahanga wa dawa za ugumba:

[…] kipindi cha pili cha serikali ya Alberto Fujimori; sera ya Taifa ya Afya ya Uzazi na Uzazi wa Mpango ilitekelezwa […] sera hiyo ilikusudia kupunga kasi ya uzazi. Uchunguzi wa hivi karibuni uliwajumuisha wanawake 2,000. Hata hivyo, takwimu na nyaraka zinaonyesha kuwa kardi ya wanawake laki tatu wa vijijini nchini humo walilazimishwa kufanywa wagumba kwa nguvu wakati wa kipindi hicho.